Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Status
Not open for further replies.
Siamini kuwa kuna kitu kama hicho kutokea lakini kama ndo hivyo ni budi Mhe. Rais kachukua hatua mara moja kumuondoa RC wa Arusha kwenye nafasi yake.
Achukue hatua kwa RC...tutasubiri.
 
Nimedokezwa kwamba video ya kipondo hicho iko mitaani , ngoja tuone kama naweza kuiweka humu jf kunogesha mambo .

Malipo ni hapahapa .
Malipo ya ubaya hulipwa kwa wema lakini ukiwa na mtu jeuri, ni bora kumlipa kwa ubaya tu.
 
Kawaida ukipigwa gumi la pua mchuzi humwagika, huyu je?
 
Hivi akipita hapa akaona anavyochukiwa anajisikiaje?
 

Kumbuka huo ni ugomvi wa ndani we mbiga, sio ugomvi na manyumbu EBO!!! (Mwenyekiti wa mkoa anaweza kuongea na mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais, na Gambo anaweza kuongea na Rais moja kwa moja ambaye ni Mwenyekiti wa Chama! UMEZIONA BUSARA ZA RCO HAPO AMA BADO!!!!!!
 
Inawezekana ikawa kweli kuwa aliambulia ngumi jiwe kwani jamaa ana matusi ya kuudhi tena wakati mwingine ya nguoni! Namkumbuka kipindi kile alichokuwa mkuu wa wilaya ya korogwe alimtukana sana yule dada aliyekuwa mwanasheria wa wilaya kuwa ana degree ya chupi! Hata ningekuwa mimi ndiye katibu ningemfuata hadi nyumbani kwake tumalizane tu kibingwa!
 
Mbona leo ameonakana akizindua mitambo ya kufyatua mitihani ya mkoa hana kovu lolote?
 
Hata kama kapigwa,shida iko wapi?!!yeye ni yesu? au Muhammad?apite hivi[emoji117]
 
Aibu hizi tutaziweka wapi jamani,Magu mbona hatukuelewi na wateule wako hawa?Hivi tuseme TISS wameshindwa kabisa kukupatia watu ambao watakipa chama na serikali taswira nzuri.Ni aibu sana kama ni kweli.
 
Hapana PM ni no.3 kwa ukubwa kisha linafuata Baraza la Mawaziri in terms of political rulling, lakini kwenye executive powers, hata ma PS kwenye wizara ndio wakuu, where executive powers lies, ndio kwenye nguvu.

P
PM ni namba 4 namba Moja Rais namba mbili makamu wa Rais namba tatu Rais wa Zanzibar namba nne Waziri Mkuu kwa itifaki ya Tanzania
 
Unaongelea itifaki ya nchi gani paskali? Hoja salute hata Mbunge anapigiwa salute, Jaji anapigiwa salute, inspector anapigiwa salute. Kwahiyo kupigiwa salute siyo hoja.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…