Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Status
Not open for further replies.
Habari kubwa kama hii bila picha ni sawa na kula mkate bila chai.



Picha tafadhali...!
 
Siyo tetesi ni kweli kulitokea sintofahamu ila ni kati ya mwenyekiti wa CCM mkoa na Mrisho, RC huyo msanii aliingia ukumbini akiwa ameambatana na maafisa hao wa takukuru na Tiss kwenye kikao ambacho akiwahusu.

Alipoulizwa kulikoni na mwenyekiti, akajibu kwamba najua hapa kuna watu wananichukia ikiwemo wewe mwenyekiti na katibu wako, kwa taarifa yenu siyo lazima niwe mkuu wa mkoa wa Arusha hata Rais akinihamisha bado nitakuwa mkuu wa mkoa.

Mrisho ni kama vile hajitambui yeye ni nani na nafasi yake ni ipi katika jamii.
 
Kuna tetesi zinadai kwamba, Mkuu wa Mkoa WA Arusha Mrisho Gambo amepokea kipigo kutoka kwa Katibu wa Ccm Mkoani Arusha Elias Mpanda Mara baada ya kulazimisha wajumbe wasiohusika kuingia kikao cha kamati ya siasa mkoa ambao yeye mkuu wa mkoa ni mjumbe lakini huku akilazimisha waingie kamanda wa TAKUKURU ARUSHA na AFISA USALAMA TAIFA MKOA ambao kiitifaki si wajumbe wa kikao hicho.

Gambo amepokea kichapo hicho na kumsababisha kuvimba pua na Mdomo baadaya ya kulazimisha wajumbe hao ambao kimsingi si wajumbe kutaka washiriki kiako na kuanza kumporomoshea matusi ya nguoni katibu wa mkoa ccm bwana Elias Mpanda,

hata hivyo baada ya kipigo kikao hicho kilichokuwa ofisi ya mkoa Arusha kilivunjika,baada ya kuvunjika mkuu wa mkoa alituma Askari wakuu akiwemo RCO wa Arusha kumkamata Katibu huyo lakini busara za RCO aliyekaa kikao na pande zote mbili kutuliza hasira zao.

Hata hivyo haijulikani kikao hicho kitafanyila lini tena huku Mwenyekiti akitafakari namna itakavyo endelea.

Gambo ambaye alipachika wagombea wake kila eneo lakini walishindwa na kambi ya mkiti aliyeshinda mh Sanare amekuwa kwenye wakati ngumu katika vikao hivyo.

Hadi sasa imekua siri kwa wanachama wa Chama cha mapinduzi Ccm Mkoa wa Arusha kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana,
Msimamo wa kamati ya siasa ni kuwa wateule na viongozi wakuchaguliwa kutekeleza ilani ya chama badala ya kuingilia maamuzi ama kuendesha chama kwa mgongo wa uteuzi wao

Gambo alifika katika kikao kikao hicho na Afisa usalama wa Mkoa Rso pamoja na kamanda wa Takukuru Mkoa Wa Arusha
Usalama wa taifa waliingizwa na Gambo kwa sababu G.Lema alisema tunajua na taarifa tunazipata kwa kila kinachofanyika ktk vikao vya ccm
 
Hahahahaha...kumbe anavyotoaga vile vitisho nguvu yake inakuaga Ni kwa Polisi. Nilitaka nishangae kwa jicho lile anaanzaje kupata nguvu ya kuzipanga na kidume mwenzake.

Mara nyingi watu wenye vitisho vingi ndo wanakuaga waoga halafu hawana nguvu.

Pongezi nyingi zikuendeee bwana Mpanda
Mpanda kampandia RC Arusha
 
Siamini kuwa kuna kitu kama hicho kutokea lakini kama ndo hivyo ni budi Mhe. Rais kachukua hatua mara moja kumuondoa RC wa Arusha kwenye nafasi yake.
 
Hii habari mpaka leo haina updates za picha wala video.
 
Ngumi ya mdomo naijua aisee mixa kuvimba hahaha
 
Usalama wa taifa waliingizwa na Gambo kwa sababu G.Lema alisema tunajua na taarifa tunazipata kwa kila kinachofanyika ktk vikao vya ccm
Huwezi kufanya kazi pekee yako.Kama ana dhamira nzuri, angewashirikisha viongozi wa chama.RSO angefanya kwa mfumo wa taasisi yao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom