Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Status
Not open for further replies.
Habari ya kupikwa hii,Katibu wa CCM Mkoa hayupo Arusha na hata angekuwepo, RC ana ulinzi si rahisi kumpiga isitoshe RC ndo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa akitoa amri iwe kwa RPC,RSO na wengine lazima waitekeleze hakuna cha eti RSO alitumia busara, amri za majeshi huwa ni utekelezaji tu na si vinginevyo huwezi kupingana na Boss wako akishatoa amri, mleta taarifa hizi za uongo inaonekana hujui majeshi yanaendeshwaje
Katibu ni boss wa RC ktk kikao tajwa na RC ni mjumbe tu . Kiprotokali Katibu wa Chama Tawala haamrishwi na RC maana Chama ni msimamizi wa Serikali , nd'o kusema Serikali ni mtoto wa Chama . RC anaweza kuwaamrisha wakuu wa vyombo vya dola mkoani mwake .
 
Ukweli ni aibu sana.ilikuwa vurugu kubwa sana ila tumieweka chini ya carpet ili Magu asijekufanya vitu vyake.
Mkuu kama habari hizo hazitakuwa na chenga, basi lazima rungu la mpingo la Magu liwashukie.
Rungu la Magu huwa halilali njaa, tusubiri na tuone!
Unakumbuka fyokofyoko za aliyekuwa mkurugenzi ama katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa RC wake kama sikosei, zilizosababisha wote waende na maji?
 
Hapa Arusha tumezoea MaRC wa kaliba ya Chalz Kileo na DC Kasapira (Mungu awaweke mahala pema Peponi!). Paskali wa JF bila shaka wawakumbuka sana hawa viongozi!
Mkuu Chuwa Albert, ulijuaje nawakumbuka RC Chalz Kileo na DC Kasapira?.

Story ukiona ndefu za aina hii, ujue huu ni utunzi, RC mkoani ndie rais wa mkoa, nani anaweza kumkatalia kitu?!. RSO na Takukuru ni kama polisi, wanaingia popote kwa mamlaka yao, wala sio kwa amri ya RC, mwanaCCM gani mwenye mamlaka ya vyombo vya dola kutimiza wajibu wake?!.

Story nyingine..nashangaa uongo huu umefika page ten!.

P.
 
Shamba ni la bwana heri,

Na mbuzi ni wa bwana heri.

basi yote heri.

Au ndugu wakigombana, we shika jembe ukalime, wakipatana rudi nyumbani upike.
 
Umeanza vizuri maelezo yako ila huko umemalizia kibashite tofautisha kuwaita kwenye vikao vya seeikali na vikao vyenu vya kimbeyambeya vya chama
Chama ndio kinaongoza serikali,kama kuna tatizo sehemu anaitwa tu Rais ameshatoa agizo hilo
Kwenye kuomba kura ni ccm ndio watakuja sio serikali,kwa ndio maana wanaitwa kutoa ufafanuzi
 
Siku ukuta ukizinduliwa asipoonekana ntajua nikwel

Ukuta wa Mererani haumhusu, ukuta unazinduliwa Manyara, yeye kipigiwa Arusha, allegedly. Awepo asiwepo kwenye ukuta haigeuzi ukweli kama kapigwa au hajapigwa.

Kiongozi ambae ukisemekana umepigwa watu wanashangilia lazima ujipime unakosea wapi.

Warioba alipigwa nchi ikalaani na kuhuzunika. Msafara wa Mkapa ulipopolewa mawe Masaki jamii ikashangilia. Tujihoji, wajipime.
 
Umesahau DC mwingine mbovu kupita wote huko Tarime! Nasikia alikuwa mwenezi wa uvccm.
 
Mkuu Chuwa Albert, ulijuaje nawakumbuka RC Chalz Kileo na DC Kasapira?.

Story ukiona ndefu za aina hii, ujue huu ni utunzi, RC mkoani ndie rais wa mkoa, nani anaweza kumkatalia kitu?!. RSO na Takukuru ni kama polisi, wanaingia popote kwa mamlaka yao, wala sio kwa amri ya RC, mwanaCCM gani mwenye mamlaka ya vyombo vya dola kutimiza wajibu wake?!.

Story nyingine..nashangaa uongo huu umefika page ten!.

P.
Kuna uzi humu unathibitisha kwamba mkuu wa mkoa ni mkubwa kuliko waziri kwa kuweka picha ya Makonda kakaa pembeni ya JPM wakati Mchemba kasimama nyuma yao. Kwa vile nchi yote imegaiwa mikoa, na kila mkoa una RC wake, itabakia hivyo tu kuwa RC kwenye zone yake anabakia kuwa juu ya waziri!
 
Nipo Ofisini kwa Gambo asubuhi hii nataka nione Nundu sijui atakuja kazini leo,ngoja nisubiri.
 
Viongozi wa ccm waliambiwa wawe wakali kuiamrisha Serikali nini cha kufanya...wametumia Maneno yake vizuri tuu
 
Mkuu Chuwa Albert, ulijuaje nawakumbuka RC Chalz Kileo na DC Kasapira?.

Story ukiona ndefu za aina hii, ujue huu ni utunzi, RC mkoani ndie rais wa mkoa, nani anaweza kumkatalia kitu?!. RSO na Takukuru ni kama polisi, wanaingia popote kwa mamlaka yao, wala sio kwa amri ya RC, mwanaCCM gani mwenye mamlaka ya vyombo vya dola kutimiza wajibu wake?!.

Story nyingine..nashangaa uongo huu umefika page ten!.

P.
Pasco unapenda picha kwa kweli, unahisi moderators hawajauona huu uzi?kama hatuna source si vizuri kupinga ama kukubali tuache ili maandiko yetu yasitutese siku za usoni.Sasa kama kilichoandikwa ni kweli kuwa RC alitukana matusi ya nguoni huoni kuwa hiyo ni provocation ambaye inaweza kumshawishi mtu kufanya kitu kisichotarajiwa? Au haiwezekani RCO kumliza kesi juu kwa juu akijua kuwa akilichukulia hilo suala official litakwenda public halafu itakuwa ni aibu kwa wateule wa Raisi.Pasco usipende watu wakuamini kama hupendi kuamini watu. Hizi verified accounts zinawatia uoga sana , maana wengi wenu mkiwa verified mnakuwa kama mtu ameokoka, Wapole kama Kardinali Pengo.
 
Watanzania tunapenda sana ushabiki maandazi, muanzisha mada kasema tetesi, hakuna proof ila watu wameshalipuka utadhani wana ushahidi wa kinachosemwa kuweni makini na matumizi ya mitandao
 
Dhambi imeanza kuwatafuna wenyewe kwanza

By the way pole yake.maana kama amevimba uso atakuwa anatisha sana.maana mimi siku zote namuonaga kama kavimba uso.sasa sijui hali ikoje baada ya kupigwa
 
Kuna uzi humu unathibitisha kwamba mkuu wa mkoa ni mkubwa kuliko waziri kwa kuweka picha ya Makonda kakaa pembeni ya JPM wakati Mchemba kasimama nyuma yao. Kwa vile nchi yote imegaiwa mikoa, na kila mkoa una RC wake, itabakia hivyo tu kuwa RC kwenye zone yake anabakia kuwa juu ya waziri!
Simtetei Makonda lakini kiitifaki Mkuu wa Mkoa ni mwakilishi wa Rais katika mkoa anakofanyia kazi
 
Pasco unapenda picha kwa kweli, unahisi moderators hawajauona huu uzi?kama hatuna source si vizuri kupinga ama kukubali tuache ili maandiko yetu yasitutese siku za usoni.Sasa kama kilichoandikwa ni kweli kuwa RC alitukana matusi ya nguoni huoni kuwa hiyo ni provocation ambaye inaweza kumshawishi mtu kufanya kitu kisichotarajiwa? Au haiwezekani RCO kumliza kesi juu kwa juu akijua kuwa akilichukulia hilo suala official litakwenda public halafu itakuwa ni aibu kwa wateule wa Raisi.Pasco usipende watu wakuamini kama hupendi kuamini watu. Hizi verified accounts zinawatia uoga sana , maana wengi wenu mkiwa verified mnakuwa kama mtu ameokoka, Wapole kama Kardinali Pengo.
Mkuu Bwana Mapesa, kuna vitu vingine, unapaswa kutumia tuu logical thinking, yaani kwa Gambo apigwe ngumi, atoke nundu, halafu huyo mtu akalale kwake?!. Kumbe sii wengi mnaotambua kilichomkuta Lema kuozea mahabusu, chanzo ni Gambo!.

Tukio hili lingekuwa kweli, by now hilo neno tetesi lisingekuwepo. Threads kama hizi ndizo zinazoshusha credibility ya jf na kutufanya sisi sote tuliomo humu kuonekana wajinga!.

Mode, please do the needful.

P
 
Kuna uzi humu unathibitisha kwamba mkuu wa mkoa ni mkubwa kuliko waziri kwa kuweka picha ya Makonda kakaa pembeni ya JPM wakati Mchemba kasimama nyuma yao. Kwa vile nchi yote imegaiwa mikoa, na kila mkoa una RC wake, itabakia hivyo tu kuwa RC kwenye zone yake anabakia kuwa juu ya waziri!
Mkuu wa mkoa ni mkubwa kuliko waziri, waziri ni mteule wa rais, mkuu wa mkoa ni mwakilishi wa rais, au rais wa mkoa. Waziri hana mamlaka ya kuviamuru vyombo vya dola, mkuu wa mkoa, anamamlaka ya kumtia mtu ndani. Mkuu wa mkoa anatembea na bendera, waziri hana. Mkuu wa mkoa anamuona rais direct, Waziri anaanzia kwa Waziri Mkuu.
P
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom