Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Status
Not open for further replies.
Duuu kweli duniani hakuna siri habari hii ishafika jf
 
Fake news; RC anayelindwa na bunduki 7.kama sio zaidi unaanzaanza vipi mpaka umshambulie kimwili kwa ngumi, teke au kichwa?! Leta picha hapa tukuelewe vinginevyo wewe ni mchochezi na sheria iko wazi!

Rais mwenye walinzi lukuki anazibwa kibao itakua RC mweye walinzi wawili!!!
 
Fake news; RC anayelindwa na bunduki 7.kama sio zaidi unaanzaanza vipi mpaka umshambulie kimwili kwa ngumi, teke au kichwa?! Leta picha hapa tukuelewe vinginevyo wewe ni mchochezi na sheria iko wazi!
Hata kama unalindwa na bunduki 200, ukileta za kuleta mbele yangu unachapwa tu sana sana nitawekwa ndani na kufikishwa mahakamani watakapoona vema; na bila kujali itachukua muda gani lakini hatimaye nitashinda kesi.

Kama hii story in ya ukweli, hongera nyingi sana kwa katibu!
 
Mkuu wa Mkoa WA Arusha Mrisho Gambo amepokea kipigo kutoka kwa Katibu wa Ccm Mkoani Arusha Elias Mpanda Mara baada ya kulazimisha wajumbe wasiohusika kuingia kikao cha kamati ya siasa mkoa ambao yeye mkuu wa mkoa ni mjumbe lakini huku akilazimisha waingie kamanda wa TAKUKURU ARUSHA na AFISA USALAMA TAIFA MKOA ambao kiitifaki si wajumbe wa kikao hicho.

Gambo amepokea kichapo hicho na kumsababisha kuvimba pua na Mdomo baadaya ya kulazimisha wajumbe hao ambao kimsingi si wajumbe kutaka washiriki kiako na kuanza kumporomoshea matusi ya nguoni katibu wa mkoa ccm bwana Elias Mpanda,

hata hivyo baada ya kipigo kikao hicho kilichokuwa ofisi ya mkoa Arusha kilivunjika,baada ya kuvunjika mkuu wa mkoa alituma Askari wakuu akiwemo RCO wa Arusha kumkamata Katibu huyo lakini busara za RCO aliyekaa kikao na pande zote mbili kutuliza hasira zao.

Hata hivyo haijulikani kikao hicho kitafanyila lini tena huku Mwenyekiti akitafakari namna itakavyo endelea.

Gambo ambaye alipachika wagombea wake kila eneo lakini walishindwa na kambi ya mkiti aliyeshinda mh Sanare amekuwa kwenye wakati ngumu katika vikao hivyo.

Hadi sasa imekua siri kwa wanachama wa Chama cha mapinduzi Ccm Mkoa wa Arusha kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana,
Msimamo wa kamati ya siasa ni kuwa wateule na viongozi wakuchaguliwa kutekeleza ilani ya chama badala ya kuingilia maamuzi ama kuendesha chama kwa mgongo wa uteuzi wao

Gambo alifika katika kikao kikao hicho na Afisa usalama wa Mkoa Rso pamoja na kamanda wa Takukuru Mkoa Wa Arusha
Tulisha sema kuwa hiyo Arusha ina wenyewe
 
Rc huwezi kumfananisha na mtu kama lema,ni mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ana dola ana mlinzi,unaanzaje kumpiga?
Eti Rco Katumia busara,Rc akisema kamata weka ndani ni amri
Halafu ccm ni chama tawala,kina haki kumuita afisa yoyote wa serikali kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kikaoni
Wacha maneno weka ndondi
 
Hahahaha [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] haya sasa hadi wana CCM wananyooshwa
USALAMA na TAKUKURU wamekuwa wajumbe wa CCM [emoji23]
Duuh mkuu au sio wew leo umecoment siasa.
 
Rc huwezi kumfananisha na mtu kama lema,ni mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ana dola ana mlinzi,unaanzaje kumpiga?
Eti Rco Katumia busara,Rc akisema kamata weka ndani ni amri
Halafu ccm ni chama tawala,kina haki kumuita afisa yoyote wa serikali kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kikaoni
Umeanza vizuri maelezo yako ila huko umemalizia kibashite tofautisha kuwaita kwenye vikao vya serikali na vikao vyenu vya kimbeyambeya vya chama
 
Yaani Katibu kanipigìa kijana wangu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom