Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Status
Not open for further replies.
Ni kweli kabisa CCM ina uwezo wa kumuita mtu yeyote kwenye kikao. Tatizo, Mrisho Gambo sio CCM, ni mwana CCM!
Huna tofauti na yule aliejitetea kashindwa kutayarisha bajeti kinzani kisa hana wafanyakazi,hiyo ruzuku mnayoletewa mnalipa watu wa kutukana mitandaoni
 
Fake news; RC anayelindwa na bunduki 7.kama sio zaidi unaanzaanza vipi mpaka umshambulie kimwili kwa ngumi, teke au kichwa?! Leta picha hapa tukuelewe vinginevyo wewe ni mchochezi na sheria iko wazi!
Ukisikia mbwa kala mbwa ndo hiyo we baki unajiuliza mwenzio ndo hivyo anauguza minundu,ndo maana Leo sijamuona ofisini kwake.
 
Kwa nini hawakuchomana visu? Daah hakuna hata aliyekuwa na kiwembe akamcharaza mwenzake bahati mbaya tena hii.
 
Hii taarifa haina viashiria vya ukweli.

Sanasana labda kutupiana maneno lakini hapo kwenye ndondi unaongeza chumvi tu.
 
Mrisho Rambo hukulusha mateke kama Rambo na komando kipensi ,kweli kifo cha nyani baunsa huzima taa
Hahahah atakuwa alikutana na mfuweni wa hatari af unajua ukipigwa header ya ghafla ata hamu ya ngumi inakata mzee unabaki kushika pua na mdomo uliopasuka.
 
Bro unashabikia fake news!
Kama fake news basi nadhani ni utabiri mzuri tui maana si unajua tena lisemwalo so ni dua njema tu wala usijali ila km ni kweli heshima kwa Katibu naziwasilisha kwa bashasha kabisa.
 
Siku ukuta ukizinduliwa asipoonekana ntajua nikwel
 
This is too good to be true.

Hii chai, mpaka umfikie mkuu wa mkoa kumvimbisha mdomo walinzi wake wako wapi?

Mkuu wa Mkoa WA Arusha Mrisho Gambo amepokea kipigo kutoka kwa Katibu wa Ccm Mkoani Arusha Elias Mpanda Mara baada ya kulazimisha wajumbe wasiohusika kuingia kikao cha kamati ya siasa mkoa ambao yeye mkuu wa mkoa ni mjumbe lakini huku akilazimisha waingie kamanda wa TAKUKURU ARUSHA na AFISA USALAMA TAIFA MKOA ambao kiitifaki si wajumbe wa kikao hicho.

Gambo amepokea kichapo hicho na kumsababisha kuvimba pua na Mdomo baadaya ya kulazimisha wajumbe hao ambao kimsingi si wajumbe kutaka washiriki kiako na kuanza kumporomoshea matusi ya nguoni katibu wa mkoa ccm bwana Elias Mpanda,

hata hivyo baada ya kipigo kikao hicho kilichokuwa ofisi ya mkoa Arusha kilivunjika,baada ya kuvunjika mkuu wa mkoa alituma Askari wakuu akiwemo RCO wa Arusha kumkamata Katibu huyo lakini busara za RCO aliyekaa kikao na pande zote mbili kutuliza hasira zao.

Hata hivyo haijulikani kikao hicho kitafanyila lini tena huku Mwenyekiti akitafakari namna itakavyo endelea.

Gambo ambaye alipachika wagombea wake kila eneo lakini walishindwa na kambi ya mkiti aliyeshinda mh Sanare amekuwa kwenye wakati ngumu katika vikao hivyo.

Hadi sasa imekua siri kwa wanachama wa Chama cha mapinduzi Ccm Mkoa wa Arusha kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana,
Msimamo wa kamati ya siasa ni kuwa wateule na viongozi wakuchaguliwa kutekeleza ilani ya chama badala ya kuingilia maamuzi ama kuendesha chama kwa mgongo wa uteuzi wao

Gambo alifika katika kikao kikao hicho na Afisa usalama wa Mkoa Rso pamoja na kamanda wa Takukuru Mkoa Wa Arusha
 
Kama fake news basi nadhani ni utabir mzuri tui maana si unajua tena lisemwalo so ni dua njema tu wala usijali ila km ni kweli heshima kwa Katibu naziwasilisha kwa bashasha kabisa.
Nimekusoma loud and clear
 
Walisha sema ukimtoa naekusumbua hiyo damu ya uasi itawatafuna na nyie mtoane mwisho wa siku mjimalize wenyewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom