Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Status
Not open for further replies.
Habari ya kupikwa hii,Katibu wa CCM Mkoa hayupo Arusha na hata angekuwepo, RC ana ulinzi si rahisi kumpiga isitoshe RC ndo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa akitoa amri iwe kwa RPC,RSO na wengine lazima waitekeleze hakuna cha eti RSO alitumia busara, amri za majeshi huwa ni utekelezaji tu na si vinginevyo huwezi kupingana na Boss wako akishatoa amri, mleta taarifa hizi za uongo inaonekana hujui majeshi yanaendeshwaje
 
Habari ya kupikwa hii,Katibu wa CCM Mkoa hayupo Arusha na hata angekuwepo, RC ana ulinzi si rahisi kumpiga isitoshe RC ndo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa akitoa amri iwe kwa RPC,RSO na wengine lazima waitekeleze hakuna cha eti RSO alitumia busara, amri za majeshi huwa ni utekelezaji tu na si vinginevyo huwezi kupingana na Boss wako akishatoa amri, mleta taarifa hizi za uongo inaonekana hujui majeshi yanaendeshwaje
Kwani ye si binadamu,alirushiwa bush viatu na alikuwa na ulinzi mkali we vepe
Ova
 
Mkuu wa Mkoa WA Arusha Mrisho Gambo amepokea kipigo kutoka kwa Katibu wa Ccm Mkoani Arusha Elias Mpanda Mara baada ya kulazimisha wajumbe wasiohusika kuingia kikao cha kamati ya siasa mkoa ambao yeye mkuu wa mkoa ni mjumbe lakini huku akilazimisha waingie kamanda wa TAKUKURU ARUSHA na AFISA USALAMA TAIFA MKOA ambao kiitifaki si wajumbe wa kikao hicho.

Gambo amepokea kichapo hicho na kumsababisha kuvimba pua na Mdomo baadaya ya kulazimisha wajumbe hao ambao kimsingi si wajumbe kutaka washiriki kiako na kuanza kumporomoshea matusi ya nguoni katibu wa mkoa ccm bwana Elias Mpanda,

hata hivyo baada ya kipigo kikao hicho kilichokuwa ofisi ya mkoa Arusha kilivunjika,baada ya kuvunjika mkuu wa mkoa alituma Askari wakuu akiwemo RCO wa Arusha kumkamata Katibu huyo lakini busara za RCO aliyekaa kikao na pande zote mbili kutuliza hasira zao.

Hata hivyo haijulikani kikao hicho kitafanyila lini tena huku Mwenyekiti akitafakari namna itakavyo endelea.

Gambo ambaye alipachika wagombea wake kila eneo lakini walishindwa na kambi ya mkiti aliyeshinda mh Sanare amekuwa kwenye wakati ngumu katika vikao hivyo.

Hadi sasa imekua siri kwa wanachama wa Chama cha mapinduzi Ccm Mkoa wa Arusha kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana,
Msimamo wa kamati ya siasa ni kuwa wateule na viongozi wakuchaguliwa kutekeleza ilani ya chama badala ya kuingilia maamuzi ama kuendesha chama kwa mgongo wa uteuzi wao

Gambo alifika katika kikao kikao hicho na Afisa usalama wa Mkoa Rso pamoja na kamanda wa Takukuru Mkoa Wa Arusha
Waache wauwane watoane roho kwa sababu wameshazoea kuuwa wengine bila ya HATIA. Angetolewa meno kabisa huyo mkuu wa mkoa akaona tamu ya madaraka. wamezoea kuwaonea chadema tu.
 
Mshasahau sheria za mtandao mkinyooshwa mnalialia una uhakika na habari yako
 
kichapo hata kapcha hamna mhhh huu uzi ni wamashaka makubwa
 
Wamepigana kama mayweather na mike Tyson...[emoji4] [emoji14]
 
Source?Picha?Video?
ushatafuniwa ufundishwe na kumeza pia, izo video na picha ni juhudi zako kutafuta na chanzo cha taarifa ndio uyu mtoa mada,

ifikie kipindi wadau wa jf tuaminiane sisi kwa sisi mtu analetewa taarifa anauliza source kwaiyo hao wenye mablog wako vzr kuliko wadau wa jf!!

muda mwingine mtu anaweza akatuletea updates yupo kwenye kikao nyeti kisichotakiwa muandishi, mpiga picha wala mchukua video, alafu mweu m1 anakuja "source, picha, video"
 
Rc huwezi kumfananisha na mtu kama lema,ni mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ana dola ana mlinzi,unaanzaje kumpiga?
Eti Rco Katumia busara,Rc akisema kamata weka ndani ni amri
Halafu ccm ni chama tawala,kina haki kumuita afisa yoyote wa serikali kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kikaoni
CCM ndo ina haki ya kumuita yeyote kuhudhuria kwenye kikao cha kamati ya siasa. Mkuu wa mkoa hana haki hiyo. Kama hii story in ya ukweli, pongezi nyingi kwa katibu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom