RC Gambo aumbuka. Vijana wa CCM Arusha wamshambulia mitandaoni, aamua “ku left “

RC Gambo aumbuka. Vijana wa CCM Arusha wamshambulia mitandaoni, aamua “ku left “

buswelu moja

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
226
Reaction score
180
Rc Gambo aumbuka,vijana wa Ccm Arusha wamshambulia mitandaoni aamua “kuleft”.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amejikuta akiumbuka katika mitandao ya kijamii hali iliyomlazimu kujiondoa huku baadhi ya vijana wa Ccm Arusha wakimshauri aache jeuri na awe karibu na vijana.

Tukio hilo lilitokea jana usiku katika kundi la Whatsapp la Arusha Youth Forum ambapo Gambo alijikuta akishambuliwa na baadhi ya vijana wa Ccm Arusha baada ya kuandika maneno kwamba “some people are stupid but lucky”akimaanisha “baadhi ya watu ni wajinga lakini wana bahati “.

Mara baada ya kuandika maneno hayo ndipo makada hao walipoanza kumshambulia huku wakimwambia ya kwamba yeye kama mkuu wa mkoa hajawahi kusaidia vijana Arusha na amewatenga.

Jimmy Pamba alikuwa kijana wa kwanza kumshukia Gambo huku akimweleza kwamba amekuwa mtu wa kujikweza na kupenda kutukuzwa.

Kabla hajajibu kijana mwingine Lucas Ngokolo aliibuka na kumwambia kwamba atamke hadharani kijana aliyemsaidia huku akimwambia kwamba amekuwa kikwazo katika mapambano ya kukusanya kodi kwani amekuwa karibu na wakwepaji kodi mbalimbali na mara nyingine huwaita wadau.

Kada huyo bila kupepesa macho alimwambia Gambo hafai kuwa kiongozi wa mkoa wa Arusha kwa kuwa amekuwa akikwaruzana na kila kiongozi anayeletwa Arusha kama wakurugenzi na wakuu wa wilaya.

Hivi karibuni katika kikao cha kuvunja baraza la madiwani Arusha Gambo aliwatuhumu mkuu wa wilaya Arusha,Gabriel Daqaro na mkurugenzi wa jiji,Dk Maulid Madeni kwamba wanamkwamisha katika utendaji wake wa kazi.

Pia itakumbukwa ya kwamba Gambo aliyewahi kukwaruzana na mkuu wa mkoa wa Arusha, Daud Ntinbenda wakati akiwa mkuu wa wilaya mpaka akaondolewa, mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti wakati akiwa mkuu wa wilaya ya Arumeru.

Hata hivyo, muda mfupi baadae aliibuka kijana aitwaye Bernad Trump ambapo alimchana na kuelezea tukio la kumweka katika mahabusu ya kituo cha polisi cha kati Arusha kwa siku tisa bila dhamana.

Trump alimwambia Gambo kwamba amekuwa akitumia mamlaka yake vibaya kuwaumiza baadhi ya watu wanaomkosoa huku akisisitiza kwamba hafai hata kuwa mbunge wa Arusha Mjini.

Akijibu mashambulizi Gambo alidai kwamba pamoja na jitihada za kuifuta Chadema Arusha kuna muda alikuwa akiishi maisha ya hofu kwani alivamiwa nyumbani kwake Muriet mara mbili na wafuasi wa Ccm kama hasira za kuifuta Chadema.

Gambo alizungumzia kwamba kila jambo baya amekuwa akisukumiwa yeye kama hatua ya mfanyabiashara maarufu Philemon Mollel “Monaban” aliponyang’anywa kiwanda cha NMC watu walipotosha kwamba yeye ndio alichangia.

Gambo alijitetea kwamba hata wakili maarufu, Albert Msando alipokamatwa na kuwekwa mahabusu Polisi kati kwa kutoa kauli kuhusu masuala ya korona watu hao hao walidai ni yeye aliamuru.

Hata hivyo, pamoja na majibu hayo Baadhi ya makada waliendelea kumshambulia kwa kumuita mnafiki na anayependa kujisikia na ndipo alipoomba kujiondoa katika kundi hilo la Whatsapp.

Gambo ni miongoni mwa watu wanaotajwa kulimezea mate jimbo la Arusha Mjini lakini amekuwa akikumbana na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya makada na viongozi wa Ccm Arusha.

Wengine wanaotajwa ni pamoja na Meya aliyejiuzulu, Calist Lazaro, mfanyabiashara maarufu, Phillemon Mollel maarufu kama Monaban, Dk Batilda Burian, Wakili Albert Msando, Edmund Mgemela, Mustapha Panju, Thomas Munisi na wengine kadhalika ambapo kwa upande wa Chadema mpaka sasa ni Godbless Lema.

Soma pia > Mrisho Gambo: UVCCM kumejaa vijana wanafiki ambao wakizeeka watakuwa Wachawi!
 
Hao vijana kweli wamejitambua sana na kuamua kumshika mkono mtu ambaye waliona kabisa kuwa anatumia urefu wa mkono wake kuwamalizia haki yao.
Rc Gambo aumbuka,vijana wa Ccm Arusha wamshambulia mitandaoni aamua “kuleft”.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amejikuta akiumbuka katika mitandao ya kijamii hali iliyomlazimu kujiondoa huku baadhi ya vijana wa Ccm Arusha wakimshauri aache jeuri na awe karibu na vijana.

Tukio hilo lilitokea jana usiku katika kundi la Whatsapp la Arusha Youth Forum ambapo Gambo alijikuta akishambuliwa na baadhi ya vijana wa Ccm Arusha baada ya kuandika maneno kwamba “some people are stupid but lucky”akimaanisha “baadhi ya watu ni wajinga lakini wana bahati “.

Mara baada ya kuandika maneno hayo ndipo makada hao walipoanza kumshambulia huku wakimwambia ya kwamba yeye kama mkuu wa mkoa hajawahi kusaidia vijana Arusha na amewatenga.

Jimmy Pamba alikuwa kijana wa kwanza kumshukia Gambo huku akimweleza kwamba amekuwa mtu wa kujikweza na kupenda kutukuzwa.

Kabla hajajibu kijana mwingine Lucas Ngokolo aliibuka na kumwambia kwamba atamke hadharani kijana aliyemsaidia huku akimwambia kwamba amekuwa kikwazo katika mapambano ya kukusanya kodi kwani amekuwa karibu na wakwepaji kodi mbalimbali na mara nyingine huwaita wadau.

Kada huyo bila kupepesa macho alimwambia Gambo hafai kuwa kiongozi wa mkoa wa Arusha kwa kuwa amekuwa akikwaruzana na kila kiongozi anayeletwa Arusha kama wakurugenzi na wakuu wa wilaya.

Hivi karibuni katika kikao cha kuvunja baraza la madiwani Arusha Gambo aliwatuhumu mkuu wa wilaya Arusha,Gabriel Daqaro na mkurugenzi wa jiji,Dk Maulid Madeni kwamba wanamkwamisha katika utendaji wake wa kazi.

Pia itakumbukwa ya kwamba Gambo aliwahi kukwaruzana na mkuu wa mko wa Arusha,Daud Ntinbenda wakati akiwa mkuu wa wilaya mpaka akaondolewa,mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya na mkuu wa mkoa wa Manyara,Alexander Mnyeti wakati akiwa mkuu wa wilaya ya Arumeru.

Hatahivyo,muda mfupi baadae aliibuka kijana aitwaye Bernad Trump ambapo alimchana na kuelezea tukio la kumweka katika mahabusu ya kituo cha polisi cha kati Arusha kwa siku tisa bila dhamana.

Trump alimwambia Gambo kwamba amekuwa akitumia mamlaka yake vibaya kuwaumiza baadhi ya watu wanaomkosoa huku akisisitiza kwamba hafai hata kuwa mbunge wa Arusha Mjini.

Akijibu mashambulizi Gambo alidai kwamba pamoja na jitihada za kuifuta Chadema Arusha kuna muda alikuwa akiishi maisha ya hofu kwani alivamiwa nyumbani kwake Muriet mara mbili na wafuasi wa Ccm kama hasira za kuifuta Chadema.

Gambo alizungumzia kwamba kila jambo baya amekuwa akisukumiwa yeye kama hatua ya mfanyabiashara maarufu Philemon Mollel “Monaban”aliponyang’anywa kiwanda cha Nmc watu walipotosha kwamba yeye ndio alichangia.

Gambo alijitetea kwamba hata wakili maarufu,Albert Msando alipokamatwa na kuwekwa mahabusu polisi kati kwa kutoa kauli kuhusu masuala ya korona watu hao hao walidai ni yeye aliamuru.

Hatahivyo,pamoja na majibu hayo Baadhi ya makada waliendelea kumshambulia kwa kumuita mnafiki na anayependa kujisikia na ndipo alipoomba kujiondoa katika kundi hilo la Whatsapp.

Gambo ni miongoni mwa watu wanaotajwa kulimezea mate jimbo la Arusha Mjini lakini amekuwa akikumbana na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya makada na viongozi wa Ccm Arusha.

Wengine wanaotajwa ni pamoja na Meya aliyejiuzulu,Calist Lazaro,mfanyabiashara maarufu,Phillemon Mollel maarufu kama Monaban,Dk Batilda Burian,Wakili Albert Msando,Edmund Mgemela,Mustapha Panju,Thomas Munisi na wengine kadhalika ambapo kwa upande wa Chadema mpaka sasa ni Godbless Lema.

Mwisho.
 
Lema acha kuweweseka muda wako umeisha
Tatizo kubwa kwa wana uvccm ni moja tu na ndiyo ugonjwa wenu mkubwa.

Mkiona mtu anawakosoa basi huyo ni cdm, hivi nyie mnajiona kama nani msiyo taka kushauriwa au kukosolewa?
 
alieiona hyo video afanye screen shot na sisi tuambulie chochote
 
Mkuu huu sio ukosoaji bali ni ubomoaji

Ni mikakati ya Lema kupata huruma
Tatizo kubwa kwa wana uvccm ni moja tu na ndiyo ugonjwa wenu mkubwa.

Mkiona mtu anawakosoa basi huyo ni cdm, hivi nyie mnajiona kama nani msiyo taka kushauriwa au kukosolewa?
 
Back
Top Bottom