RC Hapi: Niwe Mbunge, nipeleke shida za Wananchi kwa RC ili anitatulie? Hakiingii akilini

RC Hapi: Niwe Mbunge, nipeleke shida za Wananchi kwa RC ili anitatulie? Hakiingii akilini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amesema kuwa hana mpango wa kugombea Ubunge, kwani akiwa Mbunge itamulazimu kupeleka shida za wananchi wake kwa Mkuu wa Mkoa ili amtatulie, kitendo ambacho hayuko tayari kukifanya.

Hapi ametoa kauli hiyo hivi karibuni, wakati akifanya mahojiano maalum na EATV na kusema kuwa mara nyingi amekuwa akitajwa na watu kwamba atagombea Ubunge, na kusema kuwa dhamana aliyopewa na Mungu kupitia Rais Magufuli ni kubwa, hivyo anao wajibu wa kuendelea kuwatumikia wananchi.

"Sioni kama kukimbilia kwenye Ubunge ni uamuzi sahihi sana, Mimi nina Wabunge 11, wakiwa na shida wanakuja kwangu, sasa mimi ninapokimbia Ukuu wa Mkoa niende kwenye Ubunge ili na mimi niwe napeleka shida kwa RC ni kitu ambacho kidogo hakiingii akilini, wananchi waendelee kuniombea na wawe na subra huko mbeleni Mungu akijalia na umri ukiwa umesogea tunaweza kwenda eneo hilo" amesema Hapi.

Aidha Hapi amewataka wanasiasa kuwa na heshima badala ya kuendelea kulaumu kwa kila kitu na kufuata sheria na taratibu hususani katika masuala ya ufanyaji wa mikutano

HAPI WEB.jpg

 
Ni kwa vile aelewi kuwa mamlaka ya mbunge ni makubwa kuliko ukuu wa mkoa. Yaani yeye anaona kwa vile Magufuli anachezea sheria ndio itakuwa hivyo miaka yote. Haha yataisha mwezi wa kumi na moja wakati wenye nchi watakapochukua nchi yao na kuweka katiba yao inayofuata sheria na haki. Ndio atajua kuwa ukuu wake wa mkoa ni zirooo
 
Masikini wafaidika wa madaraka ya Magufuli, wanaamini katika Jesus fake na sio katika katiba tena.
Jamani MaCCM muwe na mazoea ya kusoma vifungu vya katiba. Mamlaka ya Ubunge ni makubwa kikatiba kuliko teuzi yoyote ile nchini.

#LISSURAIS2020
 
Hawana jinsi. Magufuli kawanyima uhuru. Ukiomba likizo ndo mazima. Na walivyo vilaza nani atawaajiri ?Kujiajiri hawawezi. Hapa ndo muone wanaowaimbia wimbo wa kujiajiri kila siku wao ndo kabisa hawawezi.

Hao Mateka hawawezi ishi ya ajira, kuepuka kufa njaa ni lzm wapigwe chapa na kuisujudia Sanamu ili waishi
 
... "huko mbeleni na umri ukiwa umesogea"; kwa hiyo ubunge ni dumping place?
 
Back
Top Bottom