PreGE2025 RC Homera amuagiza DC Mbarali kumsweka ndani mkandarasi endapo hatakamilisha mradi mpaka Juni 30, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wakuu

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Juma Zuberi Homera amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mbarali kumweka Ndani Saa 48 Mkandarasi anayejenga daraja la Mto Ruaha mkabala na Itipingi-Mkandami endapo atashindwa kukamilisha Mradi huo mpaka ifikapo June 30,2025

Ameyasema hayo Leo akiwa Wilayani Mbarali akikagua Ujenzi wa Daraja hilo ambalo Wananchi Wamedai Kukamilika kwake kutawasaidia kuepukana na Changamoto zilizokuwa zinawakabili kwa muda mrefu.

Pia soma: Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Wananchi Wamesema wamekuwa wakipata shida ya Namna ya kupata Mahitaji Yao ya Msingi ikiwemo huduma za Afya hasa wakati wa masika ambapo Maji hujaa eneo lote na kulazimika Kupita Barabara ya mbali ambayo mara zote imekuwa ikigharimu Ustawi wa Afya zao wengine mpaka Maisha Yao.

Aidha Dkt. Homera ametoa wito kwa Wakandarasi wazawa kuwa wazalendo na waaminifu katika Utekelezaji wa Kazi wanazopewa na kulaani vikali Tabia za baadhi Yao kutokamilisha Makusudi kwa kuamini kuwa Kazi hizo ziko vijijini Ndani Ndani kwamba Serikali haiwezifika.

Ziara za Wilaya kwa Wilaya Kata kwa Kata Kijiji kwa Kijiji na Mtaa kwa Mtaa bado zinaendelea Ndani ya Mkoa wa Mbeya zikiongozwa na Dkt.Juma Zuberi Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

View attachment 3357662
Siasa inatumaliza
 
Back
Top Bottom