Pre GE2025 RC Kihongosi; CHADEMA fanyeni Siasa za kistaarabu, tusibaguane kwa itikadi za vyama vyetu

Pre GE2025 RC Kihongosi; CHADEMA fanyeni Siasa za kistaarabu, tusibaguane kwa itikadi za vyama vyetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani Simiyu kuepuka kugawanywa kwa itikadi za vyama na badala yake kudumisha Amani na mashikamano baina ya Watanzania.

Kihongosi ametoa rai hiyo alipozungumza na viongozi wa Chama hicho Wilayani Itilima alipokuwa katika muendelezo wa ziara yake Wilayani humo kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi, leo Novemba 16, 2024.

Amewataka kuhakikisha kuwa Wanafanya kampeni za kistaarabu muda wa kampeni utakapofika pamoja na kuepuka lugha zisizofaa wakati wa kampeni ili kudumisha amani na itulivu katika kipindi hicho.
Snapinsta.app_466980492_1365969348145639_2131341346763370595_n_1080.jpg

Snapinsta.app_467421505_438643002357318_459786653104173874_n_1080.jpg

Screenshot 2024-11-16 160215.png
 
Back
Top Bottom