RC Makalla atoa Wiki moja kukomeshwa biashara ya ngono, awataka Polisi kuvaa kiraia na kujifanya wateja

RC Makalla: Atoa Wiki moja kukomeshwa biashara ya ngono, Aelekeza Polisi kutuma Askari waliovaa kiraia na kujifanya wateja. Hiyo ni taarifa kutoka mtandao wa bongo5.com hii leo.

RC Makonda alikuwa na programu za kuwasadia single mama, wajane, kufanya usafi mwisho wa mwezi, kupima tezi dume n.k

Mara nyingi tumeshuhudia matamko na mipango ya namna kutoka kwa ma RC na ma DC hii lakini inafikirisha zaidi pale ambapo yanatolewa na mtu anayengoza mkoa muhimu, tegemeo sana katika nchi na maarufu duniani kama wa Dar.

Viongozi wetu wengi wanajua uhitaji au vipaumbele vya taifa letu kwa sasa na serikali iliyowapa dhamana ya madaraka au hivi ndivyo vitu raia wengi wanapenda kusika?
 
Wanunuzi wa ngozi zao tupo poa yeye inamuuma nini?
Nalog off
 
Biashara Kongwe ulimwenguni haiwezi kusambaratishwa kwa matamko ya Oya oya. Hapo ni kuendelea kuwatafutia polisi fursa ya kuendelea kula tunda ki masihara (Burebure). Mh. makalla unahitaji mshauri makini haswa kwenye agenda unazotaka kuzisimamia na kuzitekeleza,
 
Hii biashara yenyewe hata watawala wa zama za giza hawakuwa na muda wa kushughulika nayo, waliipuza kabisa, inashangaza kuona mtawala wa karne ya 21 akiifanya ni ajenda yake.
 
Ujinga mtupu!

Huyu mkuu wenu wa dar hana kazi za kufanya?
 
Ukahaba ulikuwepo kabla hata ya yesu na muhamadi na waliikuta wakaiacha

Yeye ni nani mpaka aongee haya?
 
Ujinga mtupu!

Huyu mkuu wenu wa dar hana kazi za kufanya?
Yeye apambane na machinga na kusikiliza kero raia


Hivi hajui hao wameokoa vifu vya wanaume na vigogo wengi tuu wasife kwa manyanyaso wanayopewa na wake zao?

Tena apambane na mengine haya hayamuhusu kabisaaa
 
Hao watakaovaa kiraia lazma wale mzigo ndio wawakamate wachache, mbuzi kufia kwa muuza supu.
 
Huyu makalla anatafuta ugomvi na wanaume wa daslam
Anataka wahuni wakamalizie haja Kwa wajukuu zake?

Viongozi wa bongo kudeal na mambo madogo madogo hawajambo!
 
Naona tunaelekea kuwa Islamic state.
 
Makala hebu maliza kwanza suala la machinga kuvamia njia za watembea kwa miguu then anza kuwasaka hao malaya wa miaka nenda rudi 😜😜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…