PostGE2025 RC Makalla: Hali ya mkoa wa Arusha ni shwari, shughuli za kijamii na kiuchumi zimerejea

PostGE2025 RC Makalla: Hali ya mkoa wa Arusha ni shwari, shughuli za kijamii na kiuchumi zimerejea

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153


Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Gabriel Makalla amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Arusha, wageni na Watalii wanaofika Mkoani Arusha kuwa hali ya ulinzi na usalama Mkoani Arusha ni shwari na shughuli za kijamii na kiuchumi zimerejea katika hali yake ya kawaida.


Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Jumanne Novemba 04, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, mara baada ya Kikao cha Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa, akisema kwamba Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga pia kuhakikisha huduma za ulinzi na usalama zinakuwepo muda wote ili kuruhusu shughuli za kijamii na kiuchumi za kila siku kuendelea kama ilivyo kawaida.


Aidha katika kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa hapo jana, CPA Makalla amewataka wamiliki wa Vituo vya mafuta kufungua vituo vyao pamoja na maeneo mengine ya biashara, akiwataka Viongozi wa serikali za Mitaa na Vijiji kuendelea kutimiza jukumu lao la kuhakikisha usalama unakuwepo wa kutosha katika maeneo yao na kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria kwa Mamlaka husika.

1762262997643.png
 
Back
Top Bottom