RC Makonda atangaza vita na wanaopandisha bei ya sukari, msako mkali kuanza kesho

RC Makonda atangaza vita na wanaopandisha bei ya sukari, msako mkali kuanza kesho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
1588594865110.png

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametangaza vita na Wafanyabiashara wanaouza Sukari kwa bei ghali tofauti na bei elekezi ya Serikali ambapo amesema ifikapo Kesho kikosi kazi kitafanya ukaguzi na watakaobainika kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu Watakamatwa na Sukari kutaifishwa na Serikali.

RC Makonda amewaelekeza Wakuu wa Wilaya zote Tano za Mkoa huo kuhakikisha msako huo unaanza kesho na asisalie Mfanyabiashara yoyote anaeuza Sukari hiyo kwa Bei ya Juu.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kubaini uwepo wa baadhi ya wafanyabiashara wanaouza Sukari kwa bei ya hadi Tsh 4,500 kinyume na bei elekezi ya serikali ya Tsh 2,600 jambo linalopelekea maumivu na gharama kwa wananchi.


Mwaka 2016, Makonda aliwahi pia kutoa kufanya msako wakati wa sakata la Sukari:

Soma - UHABA WA SUKARI: Paul Makonda aendesha msako, tani 4 zakamatwa Kinondoni - JamiiForums
 
Bei ya mafuta je?

Bei ya mafuta katika soko la dunia imeshuka mpaka zero. Tanzania bei bado ipo juu ni kwasababu serikali inapata kodi kubwa bei inapokuwa juu.

Kwanini bei ya mafuta isipungue kufatana na ya dunia ili uzakishaji wa viwandani ushuke? Bei ya mafuta ikipungua hata usafirishaji wa sukari gharama zinashuka na bei lazima iwe chini.

Hii vita serikali ya magufuli haijawai ishinda na matokeo yake sukari bei hupanda zaidi.

Serikali haizalishi sukari. Viwanda sasa vinazalisha kidogo kutokana na kuwa mashamba yamejaa maji, hivyo basi uvunaji ni mgumu sana. Na kipindi cha mvua nying, sugar content huwa kidogo kwenye miwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfuko wa kgs 50 unauzwa kati ya 147k hadi 150k wao wanalazimisha retailers wauze 2,600 kwa kilo. Hiyo si biashara kichaa.

Kama yupo serious kweli aanze kukamata hao wanaouza jumla sio hao wa viduka vya mangi na wapemba
 
Bei ya Jumla sikuri kiroba cha kg 50 ni 138000 alafu unataka kg 1 iuzwe kwa 2600 kama bei elekezi? Hivi hizi ni akili au ukichwaa huu??

Kaleteni kwanza sukari ya kutosha ili nei ya Jumla ishuke ndio muweke hiyo bei elekezi.

Huu ujinga utaisha lini?
Kama mmeshindwa kuzuia mipakani sukari yote ya ndani inatoroshewa Kenya na Uganda huko kwenye njaa mnataka kumlaumu nani Sasa??
 
huyu jamaa hakuna jambo analoweza kufanikiwa hata kwa asilimia kumi
 
Jambo zuri.Nimeipenda hiyo Barkoa yake iko stylish,ningewashauri wale washonaji wa barakoa washone amabazo zimekaa kimtindo flani hivi,ili mvaaji asijisikie vibaya bali ajihisi kama vile amevaa kitu flani cha kupendezeza,tukubali au tusikubali haya maisha ya Barkoa hayataisha leo wala kesho tunahitaji kuwa wabunifu...
 
Kwanini amevaa barakoa wakati mkuu wa nchi ameshasema hakuna CORONA na hata mkuu mwenyewe havai.

Ina maana hawa wateule wake hawataki na wanapingana na kauli za rais kuhusu kuishinda vita hii ya Corona?

Hawa ndiyo wanawajaza wananchi hofu na kufifisha juhudi za rais.
 
Hili la sukari, lawama zote ni Kwa serikali, Kwa nini kila mfungo wa Ramadhani pekee sukari huwa ni adimu na kuleta mgogoro Kati ya serikali na wafanya biashara? Kwa nini huwa haijifunzi na kuwa makini Kwa vipindi hivyo?

Kwa nini serikali hata inapofanya msako wa sukari huvamia wafanya biashara wa maduka ya rejareja badala ya kwenda kwenye shina lenyewe?
 
Zanzibar bei ya juu kabisa kwa reja reja ni 2000. Ruhusuni sukari ya kiwanda cha Mahonda cha Zanzibar iletwe Tanzania bara bei ipungue na huko.
 
Na hili pia litamshinda.......Bei ilikuwa 1800 wakati jiwe anachukua nchi na akatoa bei elekezi lakini aijawahi kushuka na inapanda,leo nimenunua sukari kwa 3400.
 
Back
Top Bottom