RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

RC Makonda amesema kwa hawajaalika wazururaji jijini Dar es Salaam maana wanaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wanaDSM kwa kuwaambukiza ugonjwa wa Corona. Amesema wabunge wanaopaswa kuwa Dar ni wale tu wenye kibali Maalum cha Spika wa Bunge.

Ikumbukwe kwamba Wabunge wa CHADEMA kwa pamoja walikubaliana kutoingia Bungeni kwa kile walichodai kwamba wanajiepusha dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya vifo vya ghafla vya wabunge watatu na watakaa karantini jijini Dodoma ili kuangalia mwenendo wa afya zao.


BAADHI YA WABUNGE WALENGWA BAADA YA KUSIKIA KAULI YA MAKONDA

Mbunge wa Kigoma Mjini na MwanaJF Zitto amjibu RC, asema
Mimi ni Mbunge wa Kigoma Mjini. Nipo Dar es Salaam. Sijakwenda Dodoma Bungeni Kwa sababu ninaamini kuwa Bunge lilipaswa kuahirishwa ili kupambana na Korona. Sitakwenda Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hana Mamlaka yeyote ya kuniamulia niwe wapi katika Jamhuri ya Muungano

Sitakwenda Dodoma. Nitakaa Dar es Salaam kwa Uhuru kabisa. Najilinda dhidi ya Korona Mimi Binafsi na Familia yangu. Ninakaa nyumbani. Ninawalinda wapiga kura wangu wa Kigoma Mjini pia. Haya masaa 24 aliyotoa Mkuu wa Mkoa yaishe kwa Wabunge ni UPUUZI. ANIGUSE.


Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa naye amshukia RC Makonda
Nipo Dar Makonda jaribu kunikamata, mpuuzi wewe

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya naye hakutaka kubaki nyuma
Wewe Bashite akili ndogo haitawali akili Kubwa usitafute kiki kupitia sisi ,sisi tupo Carantini tunajitambua, utaishia kukamata wabunge wa Chama chako na Mawaziri wenu ambao hawatulii Dodoma .Anza na Waziri wa Afya si Anakuwaga Dar ,kamata kama mzurulaji ..Acha kujitutumua .

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche naye akaamua kuibuka na Mistari ya Biblia
Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,
ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,
hutauondoa upumbavu wake.
Mithali 27:22


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akaamua kukumbushia kisa cha Mwamwindi kumuua Dkt. Kleruu
Kuna wakati nilisema hawa watoto wakiachwa waendelee hivi kuna siku wata chukua wake za watu kwa nguvu.Ujinga,kiburi utaingiza Nchi kwenye machafuko.Leo nime ikumbuka kesi hii,Republic vs Said Mwamwindi ya mwaka 1972.Said Mwamwindi alimuua RC Wilbert Kleruu

Kwamba imefika mahali RC Paulo anaweza kuwapangia watu tena Wabunge wapi wana stahili kuwa?Nani anawapa huu ujasiri?tunako elekea ni kubaya sana?Kwamba Wabunge wana fananishwa na Changudoa na wazururaji halafu Bunge litakaa kimya kwa sababu wanao fananishwa ni CHADEMA? HATARI SANA


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amejibu
Niko zangu DAR napata supu ya PWEZA ... Bashite is just a CLOWN


====

WABUNGE WAZURURAJI KUONDOSHWA DAR BAADA YA SAA 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo May 06 ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam "kula bata" kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura Usiku.

RC Makonda amesema Mbunge anaepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye Kibali au Ruhusa ya Spika wa Bunge tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Hakuna asiefahamu kuwa sasahivi tuko katika Mapambano dhidi ya Virusi vya Corona na sio uzururaji, ifahamike huu sio Mji wa wazururaji hivyo natoa Masaa 24 kwa Wabunge wote kurudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la Uzururaji kama tunavyowakamata Machangudoa" alisema RC Makonda

Aidha RC Makonda amesema kwa Sasa ni kipindi muhimu cha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali na wananchi waliwachagua kwenda kuwawakilisha Bungeni na kupigania maslahi yao hivyo kitendo cha kukimbia Vikao vya Bunge ni kutowatendea haki wananchi waliowachagua.

Hata hivyo RC Makonda amesema kinachomshangaza ni kuona Wabunge hao wamekimbilia Dar es salaam kufurahia Maisha badala ya kwenda Majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na Mafuriko.

Pia soma > Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2


 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.
Hii Corona Mungu atuepushie mbali.......vituko vimezidi sasa!
 
Mliopo Dar hebu tuambieni, korona imeisha na hali ni shwari kabisa huko, maana tunaona wachunguji sasa wanawaambia waumini wasivae barakoa, leo kuna uzinduzi wa msikiti wa mtoro, daladala watu wameanza kugombania, vp kwani, kakorona kameshasepa? au mzigo wa madagascar ushatua ndio maana jeuri inapanda?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam kuhakikisha wanarudi bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji. Mbunge anaepaswa kuwa Dar ni mwenye Kibali cha Spika tu.
IMG_20200506_114913.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

Ukitaka kichekesho kama Hilo bonyeza *CCM2020#
 
Back
Top Bottom