Salaam Wadau,ni Leo tu nilipokuwa katika zururazurura yangu mitandaoni ndipo nikakukatana na clip kadhaa zikionyesha mahojiano yaliyofanywa Kwa mama mmoja akiwa na mwanae ambae anadai kuwa ni mtoto WA gwajima huyuhuyu askofu
Katika clip hizo mama yule anadai kwamba gwajima alimshawishi kufanya nae mapenz Kwa ahad nono za kumboreshea maisha yake lakini akaenda mbali zaidi Kwa kudai kwamba katika madhabau ya gwajima chini yake Kuna vyumba ambavyo gwajima huvitumia kufanya mapenzi na mabinti wengine pia WA kanisa Hilo.
Kuibuka Kwa hili kipindi hiki hakujanistua Sana hasa kwakuwa tayar gwajima yukl katika vita ya maneno na mkuu WA mkoa na pengine vita hii imefikia huku,kilichonistua ni kwanini gwajima amekuwa akikutana na tuhuma za Aina hii zaidi ya maramoja?lakini pia kwanini amekuwa akinyooshewa vidole kwenye kashfa za hovyo tofauti na wadhifa aliona katika jamii kama kiongoz WA kiroho?lakini pia ni kwann viongoz Hawa WA kiroho Kwa miaka y karibun wamekuwa wakijikuta katika kashfa mbalimbali kama hizi za ngono na mambo mengine ya kidunia?
Ikumbukwe muda si mrefu gwajima huyuhuyu alihumiwa vikali na bwana Emanuel mbasha kuwa anajihusisha kimapenzi na mkewe flora mpaka kumtia mimba na kuvuruga ndoa Yao tuhuma ambazo pamoja na ufundi WA gwajima kujibu tuhuma kila anaposhambuliwa alizikalia kimya kabisa,pia mbasha alienda mbali mpaka kufikia kumkana mtoto aliyezaliwa na flora akisema ni WA gwajima napo gwajima hakuwah kukanusha Hilo.
Juzikati akahusishwa pia na tuhuma za biashara za dawa za kulevya na Sasa hili jingine LA ngono nalo limeibuka,Ikumbukwe pia gwajima si kiongoz pekee WA kidini kuwah kuhusishwa na ngono,wapo pia kina geor Davie ambae alihusishwa kupora mke wa mtu huko arusha,yupo pia mchungaji mwingira ambaye alishitakiwa mahakamani na mtu aliyedai nabii huyo na mtume alimbaka mkewe,zipo pia tuhuma za chinichini zikimhusisha askofu pengo kuwa Ana watoto aliozaa Kwa siri na mwanamama flan ambaye anahusiana nae Kwa siri
Ndugu zangu Kwa kuzingatia kwamba ndugu yetu gwajima na viongoz wenzake wameshawah kuwa watuhumiwa WA kukosa uadirifu ni vyema bas tusimchukulie dhamana moja Kwa moja Bila yeye kututhibitishia Kwa ushahidi WA vipimo kwamba hajampachika mimba hiyo huyo mwanadada,ndipo hapo naposema bashite alete vyeti na gwajima nae apime DNA atuletee vyeti vya majibu ya DNA toka Kwa mkemia WA serikali tujilidhishe kuwa nae Hana walakini katika uadirifu wake.
Karibuni Wadau tuchangie kuhusu hili