RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

mange akiichukua issue ya Ben ni sekunde tu info Zote tunazipata
Aichukue hayo mavyeti mtajuana na Ndalichako mie nimejikuta nakosa amani kwa Ben kutoweka tuu na sie kujisahaulisha....

Kuna wakati nahisi hili wamelileta ili tumsahau Ben.
 
Sizonje Mungu anakuona.. Haya yote yanasababishwa na wewe... Ubabe huu kamwe hauvumiliki.. Nchi imekua ya vitisho kila kukicha.. Sizonje unapewa nini na Bashite? huu sio uongozi sasa.. Sauti ya wanyonge uliyotuzuga no wanyonge wepi.. Bunge lako tukufu linadharauliwa na kusononeshwa,..ukumbuke na wewe uliwahi kuwa mjengoni pale. Chombo chako kile cha habari ukipendacho leave dhati Kama ulivyotuambia,watangazaji wanapigwa mitama, uko kimya... Vyeti havijaletwa mpaka dk hii..huku wengine ukiwa umewaweka ndani (jela).. Baba wa wanyonge uko kimya ...kunani?
 
Habarini wana Jamvi tangu jana usiku mjadala wa Makonda ulipozuka kuhusu kuvamia ofisi za Clouds Media nilikaa kimya sikuchangia chochote kwasababu nilitaka kupima ukweli wa Jambo lenyewe.

Maana Makonda anaweweseka kweli anapiga simu kwenda kwa watu mbalimbali wa karibu na Mh Rais sijaelewa kwanini anafanya yote hayo.

Ila nimejiridhisha kwa kupata ukweli juu ya jambo lenyewe kuna mpango mkakati uliochorwa na Makonda pamoja na timu anayoshirikiana nayo.

Mpango wake anataka kubadili taarifa hizi kwa kusema Usiku wa Ijumaa walikwenda ofisi za Clouds Media kwa ajili ya kupata material ya kipindi walichorekodi katika sherehe ya mwaka mmoja wa Makonda pale Ukumbi wa Polisi Oysterbay.

huyu kijana ni msaaidizi wa Mkuu wa mkoa nilimpokea kipindi ametoka mafunzo nafikiri naye alishiriki kwenye huo Uvamizi ofisi za Clouds Media.
 
Suala sio kumuamini mange video ipo na makonda kaonekana anaingia na wanajeshi.....ila mange kiboko nahisi clouds wameiachia makusudi video baada ya mange kutishia kumwaga siri za maboss wa clouds!! Ila makonda ni kilazaaaa anajiona rais wa hii nchi au yaan nazidi kumchukia
Hao clouds kama wana mambo mabaya wayafanyayo ambayo Mange anayajua wasitegemee kuvuja kwa video hiyo kutawafanya wawe salama...

Ni zamu tuu wataumbuka wakati ukifika
 
SOMA EPISODE 2, POST # 282
SOMA EPISODE 3, POST # 655
SOMA EPISODE 4, POST # 852
SOMA EPISODE 5, POST # 1115 Click to expand..
 
naomba aliyeona mitutu purukushani na uvamizi kwenye hiyo video anieleweshe . naona video ya sekunde kumi na tano mtu kafungua mlango kaingia basi . labda kama iko nyingine mie sijaiona lakini haya mambo ni mazito siyo ya kuleta clip ya sekunde kumi na tano ambayo hata haionekani sawasawa alafu ndiyo itupitishie weekend hadi tunasahau kuwa yanga na azam wametoka kimataifa
 
we kiazi kweli kwani uvamizi hadi muwe wangapi
Ni kweli clip inaonyesha watu wanaingia kistaarabu bila purukushani yoyote ile makonda anaulinzi so haina utata wowote sema clouds wanataka kuzima soo wasionekane wabaya hata mara ya kwanza basi wasingerekodi baada ya kuona hawana uhakika na taarifa hiyo
 
Hiyo video clip niliyoyaona ni fupi sana na inaonesha watu wawili na askari wawili.

Sioni uvamizi wowote hapo.
kimetoka kipande hicho kwanza, akanushe vitolewe vingine, swala bado hot, Gwajima anasema vipande vyote anavyo kwanza anawasubiri Clouds waseme, ila kuna wahusika waliopigwa na vitako vya bunduki ili kutoa tape
 
Hii ishu inayoendelea ya makonda kuvamia clouds na silaha kama ipo basi ni mkakati uliopangwa kabisa ili jamaa aweze kutumbuliwa na kosa la kutumia vibaya madaraka kwa kuvamia kituo cha habari na silaha na akitumbuliwa kwa kosa hilo bado litamuweka Makonda kwenye safe side ya yeye kuweza kurudi baadae kwenye medani hii ya uongozi au siasa kwani wengi tumeshaona wakitoka kwa makosa tofauti na kurudi kwenye vipindi vingine kwa sera fulani ya kuwa walionewa mwanzo au walifanya ili kulinda kitu au sababu nyingine...
HII ITASAIDIA KUTOTUMBULIWA NA VYETI FEKI KWANI TUHUMA HIYO INAMUHARIBIA IDENTITY YAKE KABISA KUANZIA JINA NA HATA MTAANI NI ZAID YA AIBU...
LAKINI HILI LIPO SO SOFT NA NI MKAKATI WA WAZI NA CLOUDS...
TOKEA LINI CLOUDS NA JAMAA WAKAKOSANA WAKTI KILA KUKICHA MUNGU WA MAGOGONI NA BASHITE WAMEKUWA WAKITUMIA KILE CHOMBO KWA MASLAHI YAO....
 
Huu Ndio ukweli wa. Mambo
 
Back
Top Bottom