Kutokana na sakata la Mh Makonda kuingia Clouds Media usiku, kila mtu amekua akisema yake. Wengi katika hao wanalaani Mkuu wa mkoa kufika pale akiwa na askari polisi wenye silaha. Wakumbuke polisi kwa kiapo chao na kazi zao ni walinzi wa amani. Sasa kila anayejipendekeza husema wanalaani Mh Makonda kuingia clouds akiwa na polisi. Kwa kauli zao Mh Makonda iwapo angefika peke yake hata kama angefanya kitu kibaya isingekuwapo dosari. Polisi waalikuwapo kuangalia usalama wa mkuu wa mkoa na wananchi wanaomhudumia mkuu wa mkoa.