RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

Kama Kuna footage au hakuna, Kama Gwajima ametelekeza mtoto au imetengenezwa kumchafua, hii Sinema inatakiwa iishe sasa Kwa Mh kutoa vyeti hadharani au aachie ngazi au aachishwe na mamlaka iliyomteua.
Niliandika hapa JF Gwajima atoe vyeti huyu bwana anaweza kuja kumbwatukia na sasa yametimia.
 
Clouds Wamejitosa kwenye Sakata la Makonda kwa gear ya hii ili kuhadaa umma kuwa walikataa kurusha kipindi ili watumie social media kama ngao yao wasionwe ushiriki wao. Too low
Kuleta JF hii meseji ni namna ile ile ya kumpa promo Makonda aka Bashite na kuleta political diversion kwa kutumia mbinu ya huyo mama aliyepigika akiwa na mtoto
Pathetic

JF moderators wameingia naona Kiana kwa kuigiza igiza kufuta thread hii huku nafsini wakitaka iendelee kwa manufaa ya Makonda aka Bashite
 
[emoji23] [emoji23] umeongeza siku zangu za kuishi[emoji106]
Yaani kila siku MAPYA hadi raha sana huu mchezo ukitaka kufaid kuwa neutral utafurahi na ROHO yako.. Leo nimecheka Sana yule mdada anasema amezaa mtoto na Gwajima ETI anadai huyo mtoto mjanja mjanja kama Gwajima Sasa Nikajaribu ku imagine asee nimecheka Sana ETI mtoto mtundu mtundu Muda wote
 
=====
Msomaji, vema pia ukasoma hapa > Mwanamama kupitia Uhuru FM, adai kuzalishwa na Askofu Gwajima na kutelekezwa!
=====

Makonda hua anafika office za clouds mara kwa mara. Siku zingine anashinda hapo mpaka jioni. Siku ya Alhamis Makonda alifika office za Clouds Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.

Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.

Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.

Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.

Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.

Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!

kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.

SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.

Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.

Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.

Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.

Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.

Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.

Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.

Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.

====
Kutoka kwa wadau wa Clouds Media
Mh kweli elimu ya makonda mkuu wa mkoa sawa na ya kwangu mimi muuza viroba vya konyagi stand msamvu
 
Mimi ni kama Tomaso, nasubiri picha au video ili nijihakikishie kuwa ni kweli.
Mi pia maana nashindwa cha kuchangia. Ila inawezekana ikawa kweli. Clips za shiwaladu huwa wanakuwa wa kwanza kupost wao. lakini hawajapost badala yake mfuta viatu wa bashite le mburulaz ndio kapost.
 
Umbea mbaya sana,KIPINDI CHA SHILAWADU hakina manufaa kwa taifa,
Huyo makonda clouds wamemlea wenyewe
 
1d179dd8ad8525373e215bae1d9b4b4c.jpg
Ndio nimefika jamvini.
 
Hii nistori ya kupika, na mtungaji yuko vizuri sana, ili niamini tofauti post picha AMA Video ya huko kutekwa kwa shilawadu wakiwa clauds media unless ni story TU!!!


Upande wapili nikwamba hii yote inalengo kututoa kwenye hoja ya msingi, MAKONDA KUJITHIBITISHA KAMA MAKONDA na vyeti original na historia ya waalimu waliomfumdisha na marafiki zake AMA kugundulika yeye kweli ni BASHITE.

Uyo mama ukimfuatilia maongezi yake utajua kunawalakin!!! Hapa lengo nikuanzisha mlumbano ya aina mbili, team tunataka DNA na Team tunataka VYETI!!!

Wakati mnaendelea na hayo malumbano, wengine wanaipiga inchi!!! Tutumie akili wa tz!!!
 
Clouds Wamejitosa kwenye Sakata la Makonda kwa gear ya hii ili kuhadaa umma kuwa walikataa kurusha kipindi ili watumie social media kama ngao yao wasionwe ushiriki wao. Too low
Kuleta JF hii meseji ni namna ile ile ya kumpa promo Makonda aka Bashite na kuleta political diversion kwa kutumia mbinu ya huyo mama aliyepigika akiwa na mtoto
Pathetic

JF moderators wameingia naona Kiana kwa kuigiza igiza kufuta thread hii huku nafsini wakitaka iendelee kwa manufaa ya Makonda aka Bashite
Ni kweli hapa clouds kuna ujanja wanafanya kukwepa Lawama za kufanya kazi kwa upande mmoja pasipo kubalance ya Gwajima kwa kisingizio kuwa Gwajima alikuwa hapatikani.
 
Back
Top Bottom