Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duuuh,hebu nipandishie kiainaPicha ya security camera imeshatoka. Wenzao si huwa wanazifunika na kitambaa au wanavunja vunja.
Mkuu heshima kwako.....Hivi ni halali hii habari kuwekwa humu? Kwani Makonda ni celebrity? Basi sawa maana na huku tumeifuata. Hatujafuata jukwaa bali tumefuata habari! Tupo na Bashite.
Hahahaa..... Wafuatiliaj mbona tupo tumejaa tele, wao waendelee tu.Hii series nahisi ina episodes 20 halafu huwez kuamini ndo kwanza tuko ya tatu.. Jana nimecheka Sana yule Dada anayedai kuzalishwa na Gwajima ETI mtoto mjanja mjanja kama Gwajima asee. Ulimwenguni raha sana
Zipo cctv camera za kituo kimoja cha redio na tv jijini Dar es Salaam zikimuonyesha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Paul Makonda akiwa anaingia kituoni hapo na askari wa JWTZ aliyebeba silaha ya moto.
Video hiyo inaonyesha kuwa ndugu Makonda anatinga kituoni hapo kwa style ya kuvamia akiwa amebatana na kijana mmoja (mtangazaji wa kipindi kimoja maarufu kituoni hapo) askari mmoja wa jeshi la polisi na huyo wa JWTZ ambaye amening'iniza silaha na anafunga mlango huku akionekana kutoa amri kwa watu ambao wamebaki nje.
Sheria zetu zinasemaje kuhusu askari wa JWTZ? Kwanini RC aambatane nae tena akiwa na silaha ndani ya kituo cha matangazo?
Yote hayo chanzo ni yule mkazi wa jumba jeupe,aliwajengea kiburiTena hatari kabisa kumkabidhi jeshi mtu asiyeaminika,mualifu wa kugushi vyeti na identity ya mtu mwingine anaweza kutumia hilo jeshi kinyume na kuhatarisha amani ya nchi. Hili ni angalizo na ni aibu kwa nchi ya kistaarabu kama Tanzania kuona matukio ya aina hii. Ni kama Tanzania kwa sasa tunaongozwa na magenge ya kihalifu.
Ninapata wasiwasi ata ofisi za JF zinaweza kuvamiwa kwa style ya clouds kuvamiwa na kuhatarisha usalama wa watumiaji. Sidhani hili kama lipo sawa. Kuna ukakasi na kinyaa ndani ya sakata la bashite.
Ata akina Iddi Amini walianzia hivi hivi wakafanikiwa kufanya mapinduzi.
Clouds kosa lao lipi?! Wao wamepata taarifa kwamba kuna habari na hawakulazia damu! Baada ya kuona habari imekosa sifa za kuirusha; wakagoma kuirusha!! Na hata walipoendewa na askari; bado hawakuirusha!!Kama habar ni ya kweli,kosa ni la Clouds Media si la Makonda (Bar Shite)
Wajitathmini
Pengine mengine anamficha.... Nahisi kam anampa wakati mgum sn.... Na wazazi piaMke wa makonda annashindwa kumshauri mumewe jamani?
Asante mkulu nimeona! Inabidi mtu ujifinye ili kuamini kuwa hauko ndotoni. Huyu mtu ni janga la Taifa.Jitahidi ufike Instagram kwa Mange kimambi
Yaan we kama mimi.... Hadi rahaDah hii ishu ya clouds imetisha mbaya kma naota vile dah
Ujinga wa ku-release CCTV footage; au?!Croud's tunaomba muombe radhi kwa ujinga mlioufanya!!
MAKONDA AVAMIA CLOUDS KWA MITUTU YA BUNDUKI : [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] CHUPUCHUPU KUUAWA.
Jengo la Clouds Media Group lililopo Mikocheni B jana lilishuhudia sekeseke la aina yake baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia akiwa na Walinzi wenye Bunduki.
Tukio hilo tukoea majira ya Usiku wakati kipindi SHILAWADU kikiwa hewani ambapo Makonda alivamia kwa lengo la kushinikiza Shilawadu waonyeshe mahojiano yenye lengo la kumchafua Askofu Gwajima.
Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba, mwanzoni wiki 2 zilizopita, SHILAWADU walipigiwa simu na watu wasiojulikana wakieleza kwamba wana 'ubuyu' mzito wa kuhusu Askofu Gwajima na mwanamke anayedaiwa kuzaa nae. Mwanzo Shilawadu walikataa habari hiyo, lakini siku moja walikutana na Makonda akawashawishi SHILAWADU wafuatilie stori hiyo. Kama kawaida yao kupenda umbea, SHILAWADU wakiongozwa na Soudy Brown walimtafuta mwanamke anayedaiwa kuzaa na Gwajima kisha wakamhoji.
Hata hivyo, kwa kuhofia nguvu ya Gwajima katika kupambana na shutuma dhidi yake, na kwa kuzingatia maadili ya kazi, SHILAWADU waligoma kurusha habari hiyo hewani mpaka wapate kauli za upande wa pili ( upande wa Gwajima ). Baada ya kuhangaika huku na kule , SHILAWADU walishindwa kupata upande wa pili wa habari ( walishindwa kubalance story ).
Kutokana na hilo, na kujua kwamba Gwajima asingewaacha salama kwa kutoa story ya uongo dhidi yake, [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] na wasimamizi wa vipindi wa Clouds Tv waliamua kuachana kabisa na story hiyo.
MAKONDA ANAINGIAJE? : Imefahamika kwamba watu ambao walipiga simu kwa Shilawadu kuhusu uwepo wa Mwanamke huyo ni watu wa Makonda. Makonda alitaka story hiyo itolewe kupitia [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] ambao wana kawaida ya kuripoti matukio ya Watoto/wanawake waliokataliwa. Kwa kuwa Makonda ana marafiki wengi pale Clouds, aliamini kwamba story hiyo lazima ingetolewa na hivyo kumchafua adui yake GWAJIMA ( kuzima sakata la vyeti ).
Akiwa nyumbani kwake Masaki, Makonda alikaa kwenye Tv yake Ijumaa kusubiri SHILAWADU wamvue nguo Gwajima. Cha kumsikitisha, Makonda alipata habari kwamba SHILAWADU wamegoma kupeleka habari hiyo. Hata viongozi akiwemo swahiba wake Ruge walikaataa kabisa kupeleka habari ambayo haiko 'balanced' na mbaya zaidi inawaingiza kwenye vita na mtu wa aina ya Gwajima.
Kama kawaida yake, Makonda aliamua kutumia ubabe. Kwa kuwa amezoea kuingia Clouds, Makonda alifahamu kuwa muda huo viongozi hawapo na watu waliopo anawamudu. Hivyo aliamua kwenda Clouds kuhakikisha Shilawadu wanaonyesha habari hiyo ya kumchafua Gwajima. Hivyo alibeba wanaume zaidi ya 8 wakiwa wamebeba silaha za moto.
Alipofika Clouds, walinzi wa Getini walimruhusu kupita yeye na gari iliyokuwa nyumba yake akisema ni rafiki zake wamekuja mara mara moja kwenye SOSOO FRESH kwani Adamu Mchomvu amewaalika. Lakini alipofika Reception, Mlinzi wa zamu alisitia baada ya kuona Makonda amekuja na watu wengi. NA HAPO NDIPO KASHESHE ILIANZA.
Walinzi wa Makonda walitoa Bunduki, walimtishia Mlinzi wakampiga sana na wakatumia nguvu kubwa hadi walifanikiwa kuingia ndani. Walipofika na Bunduki zao, Makonda aliamuru kila mtu kukaa alipo huku akilazimisha habari ya Gwajima iende. Kwisa kama kiongozi wa kipindi ndiye ambaye alipingwa mitama na ngumi za kutosha.
Kwa walioangalia kipindi wanajua kwamba kipindi hakikuisha, hiyo ni kutokana na kwamba Makonda na waligawa kipigo cha maana kwa Shilawadu kisha wakawabeba kwenda nao nje akisema wanaenda Cental.
Pia alitumia Bunduki kuwalazimisha Shilawadu wampe Video ya Mama anayedaiwa kuzaaa na Gwajima ( alipewa ). Makonda aliwaambia wapambe wake kama Shilawadu wamekataa kuonyesha habari hiyo baasi yeye atahakikisha inasambaa kupitia mitandao ya kijamii.
Hivi sasa Shilawadu hawako sawa kisaikolojia huku Suod Brown akiwa hana amani kwani alipigwa picha na Makonda alimuambia kama anaogopa kumdhalilisha Gwajima baasi yeye atadhalilishwa kwani Sura yake itawekwa hadharani kila mtu afahamu.
Baadae Makonda aliondoka baada ya kupigiwa simu ambayo haijulikani nani alipiga lakini Makonda alipoondoka Ruge alingia Clouds akiwa na watu huku na yeye amebeba bastola. Inaaminika ile simu ilipigwa kumuambia aondoke maana Ruge anakuja.
Source : Hidden.