RC Makonda: Bei ya vinywaji itashushwa kwa masaa 6 Dar kama Taifa Stars itaishinda Uganda

Nimesema sana kuwa kumuweka Makonda kwenye mambo ya kuhusu nchi ni kuitia unajisi nchi na kuleta balaa lisilozuilika.
Hili tangazo lake kuwa Stars wakishinda eti pombe itauzwa kwa nusu bei kwa masaa sita haliina mashiko kabisa na halifai kwani huwezi kuwashirikisha watu waiombee Taifa Stars kwa Mungu kupata ushindi kasha ili munywe pombe sana kwa vile inauzwa nusu bei.
Hakika kama kuna jambo tutajutia ni kumpa jukumu kama ti hiyo Makonda! Makonda ni balaa la uhakika kwa Stars na kuna kila dalili tukachezea kichapo nyumbani.
 
Ambao walipaswa wapewe hiyo kazi wapo pembeni mfano Ali Mayay, Lunyamila, Pawasa , Matola n.k
Unamuweka sijui wema, mara shilole sisi akili zetu sijui wapi zinakwama
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani atakayefidiahilo punguzo? Au mimi sijaelewa Je watu wa mikoani wenye mapenzi na Timu yao nao watafikiriwaje.. Ndiyo maana nina walakini ni hii kamati ya Ushindi
 
Ambao walipaswa wapewe hiyo kazi wapo pembeni mfano Ali Mayay, Lunyamila, Pawasa , Matola n.k
Unamuweka sijui wema, mara shilole sisi akili zetu sijui wapi zinakwama

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na wewe...

Ndiyo tatizo la kurukia fani za watu....

Hii no soka,tungewaona hao uliowasema au akina Tino, Mogella, Chambua, Pondamali, Malota, Masatu nk.... sasa eti Shishi bebe sijui hao eti wanaowaita mastaa... !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…