RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

Nadhani Wwnanchi tunaonekana ni Mazuzu wa Kiwango cha juu!
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Paul Makonda amenena yake kuhusu hali ya Corona mkoani Dar es Salaam. Akizungumza na vyombo vya habari amesema hali sasa inaelekea kuwa shwari, idadi ya wagonjwa inazidi kupungua na kuwatoa hofu wakazi wa mkoa huo.

Vile vile amesema alifanya uchunguzi na kugundua watu wenye nia ovu mtandaoni walinunua majeneza na kwenda kwenye maeneo ya makaburini na kuchimba chimba na kujifanya wanazika ili kuleta taharuki.

Kama hali ni shwari basi fungueni shule na vyuo tumechoka kucheza na watoto majumbani: akili za kwambiwa changanya na za kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hali imekuwa shwari siyo kama ilivyokuwa awali...kwani hali imeshawahi kuwa mbaya????????/mi nilikuwa sijui kama serikali ilipitia hali mbaya hapo nyuma
 
Makonda hiyo idadi ya wagonjwa iliyopungua imetoka wapi wakati mnasema, maabukizi yapo kidogo sana....I see na nyie viongozi mambo yenu kiboko!
 
Hii nchi ngumu sana. Kweli watu wanunue majeneza kabisa kwa ajili ya kuigiza kuzika?
Kama waliandaa magari mabovu na petroli ili wayalipue baada ya uchaguzi 2015 wakiwa na lengo la kutaka kuiaminisha Tanzania pamechafuka kutokana na mauaji ya watu wengi kwa kutumia hiyo milipuko ya hayo magari ndani ya kariakoo hivi unadhani watashindwa kununua majeneza? Achani kushabikia wapinzani, wana ajenda ngumu sana sema wengi mnashabikia kitu msichokijua, na mshukuru umahili na uzalendo wa vyombo vyetu vya ulinzi, lasivyo nchi hii leo tungekuwa pabaya.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Paul Makonda amenena yake kuhusu hali ya Corona mkoani Dar es Salaam. Akizungumza na vyombo vya habari amesema hali sasa inaelekea kuwa shwari, idadi ya wagonjwa inazidi kupungua na kuwatoa hofu wakazi wa mkoa huo.

Vile vile amesema alifanya uchunguzi na kugundua watu wenye nia ovu mtandaoni walinunua majeneza na kwenda kwenye maeneo ya makaburini na kuchimba chimba na kujifanya wanazika ili kuleta taharuki.
👏👏👏👏👏​
 
Back
Top Bottom