kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Wakuu amani iwe kwenu,
Rais Magufuli mara nyingi amesisitiza watu kuvaa barakoa ili kujilinda na kulinda wenzao dhidi ya kuenea kwa ugonjwa hatari wa corona. Rais amesisitiza sana hili na nilitegemea viongozi wa chini akiwemo Mkuu wa Mkoa DSM, Wakuu wa wilaya zote, Kamanda wa kanda maluum ya DSM na Wakuu wa polisi wa Mikoa ya kipolisi zote za DSM wamsaidie mheshimiwa rais kuhakikisha agizo hilo la watu kuvaa barakoa linatelekezwa vyema ila wapi.
Leo ukipanda daladala ya kwenda popote DSM utakutana na watu wachache sana wamevaa barakoa inavyopaswa, wengine wanavyo wamevaa ila kaacha pua nje, mwingine anayo ila kaishusha chini ya kidevu, mwingine anayo ila kaiweka kwenye paji la uso, mwingine kaishikilia mkononi tu na wengi hawana kabisa.
Sasa kama mheshimiwa Rais kasema watu wavae barakoa halafu wanakaidi kuvaa huku wakijua wanaweza kueneza au kupata kwa kutokuvaa halafu nyie viongozi wa chini nao mko kimya mnategemea nini?. Ina maana RC Makonda na kamanda Mambosasa hamjui kwamba watu wanakaidi hii amri halali kiafya tena ombi la mheshimiwa rais ambalo ni amri kabisa kama mnavyotuamisha kila siku?
Hivi kwanini viongozi wetu mnapenda kiki tu kwenye mambo ya kisiasa badala ya haya mambo ya muhimu? Juzi kuna vijana wa CHADEMA wamekamatwa huko sijui Iringa kwa kugawa barako badala ya polisi kushughulika na wasiovaa barakoa. Hivi ni lini Mheshimiwa rais kakataza chama, au raia kuchangia barakoa au ndoo za maji? Kama ipo mimi sijasikia ila nimesikia akisema watu wavae barakoa. Sasa wa kumkamata ni nani? Anayegawa barakoa kukinga watu au anayekaidi kuvaa tena kitu cha sh 500 hadi 1000 na kibaya wakati mwingine anayo mkononi.
Rais alipotangaza kusitisha maandamano na mikutano ya hadhari mpaka 2020 kila RC na RPC aliitikia kwa nguvu zote hadi vikao vya ndani ambavyo hamkuambiwa kukataza lakini kwa hili la Corona mko baridi huku watu wakiendelea kuambukizana, mnataka Mheshimiwa Rais aseme kwamba kuvaa barakoa ni sheria na ambaye hatavaa atawajibishwa ndiyo muanze kazi?
Kama kila kitu mpaka muambiwe mnasubiri nini huko ofisini? Tena cha hatari ni kwamba traffic wetu hawajali kuhusu kondakta, dereva wala abiria asiye na barakoa (pongezi kwa traffic wachache wanaokumbusha watu). Kuhusu barakoa kusiwe ni utani iwe ni sheria na itekelezwe kwa hiari na shuruti kwa asiyetaka hasa kwa DSM.
Watu wa TEMESA pale Ferry mwanzoni mliweka vijana wa SUMA JKT kusimamia unawaji na kulazimisha watu wavae barako kabla ya kuvuka, upande wa barakoa naona mnajitahidi japo wengine bado wanakadi ila kuhusu kunawa kumeshakuwa kama hiari tu wengine hawanawi japo maji yapo kwasababu vijana wa suma hawasimamii tena.
Chondechonde Mkuu wa Mkoa na Ndg. Mambosasa, tusaidieni kuwashughulikia bila huruma wanaokaidi kuvaa barakoa, hii iwe sheria halali yenye adhabu kali. WHO wanasema huu ugonjwa lazima tujue namna ya kuishi nao sasa kama wakati huu walau mikusanyiko inakatazwa na shule zote zimefungwa watu hawavai barakoa wala kunawa pale tutakaposema jamani huu ni ugonjwa wa kudumu tuishi nao hivyo hivyo kama UKIMWI nani atavaa barakoa? nani atanawa? watu wataendelea kupiga chafya na kukohoa kama mbuzi .
Nasisi Watanzania sijui tukoje jamani kusimamiwa hadi kwenye vitu vya kawaida kama kuvaa barakoa, huko kwa wenzetu wanaoanza kuruhusu shughuli ziendelee wana akili , wanasikia na kufuata ushauri wa watalaamu ila huku kwetu ni changamoto tuna jamii za watu wajinga wasioelewa wala kutii mamlaka.
Nb: Suala la Corona ni la mtu binafsi kisha la familia halafu baadaye la taifa ukifa wewe hasara ni yako na familia yako chukua tatua kemea anayetaka kukuambukiza kwa kutokuvaa Barakoa.
Kindikwili.