RC Mara awaondoa Makatibu wa Wabunge kwenye Kikao, adai wao si Wajumbe wa Kikao hicho

RC Mara awaondoa Makatibu wa Wabunge kwenye Kikao, adai wao si Wajumbe wa Kikao hicho

Sasa kama hawahudhurii vikao mikoani kwao,wao wanawakilisha nani,nini na maeneo gani!!????
Wabunge hawa ni viazi na wabinafsi sana.
 
Mazoea hujenga tabia. Hii itawafanya wajirekebishe. Hivi hata kwenye vikao vyenye posho huwa wanatuma makatibu wao?
 
Huyu RC yupo serious na kazi yake, amewakataa wahuni.
 
Yupo sahihi. Wabunge wenye tabia kama hizo wanapaswa kuitwa kwenye kamati ya maadili ya bunge inapobidi.
 
Hicho kikao posho ni kiasi gani?
posho 250000, kuna perdiem transport allowances kwa wale wanaotoka nje makao makuu ya mkoa (transport allowances ni lita za mafuta kutokana umbali) kuna wanaovu zaidi ya m 1 .
Ma Ded na Ma dc wanaweka mafuta ya ofisini ya kuwawezesha kwenda na kurudi hadi perdiem wanajilipa ofisini kwao wakifika huko hizo za kikao wanazitia mfukoni.
Vikao hivyo ni Road board na RCC .
Posho za vikao hivi zikifanyiwa uhakikI zitaibua madudu ya kufa mtu (perdiem inatolewa kwa mjumbe wa kikao+ dreva wake na katibu wake kwa wabunge)
 
Back
Top Bottom