RC Mnyeti: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato ni mnafiki, mhuni na muongo!

RC Mnyeti: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato ni mnafiki, mhuni na muongo!

Watumishi kukemewa ni ushamba? Unakula kodi za wananchi kama mali ya baba yako alafu watu wakae kimya?
Hizo lugha alizotumia ni za kukemea ulaji wa Kodi? Anayefuja Kodi anapelekwa mahakamani na sio hizo chuki binafsi ili kusaka sifa za bei rahisi.
 
Tumia akili. Nazungumzia wakati hayati akifokea wazembe alikuwa akifanya kazi kama mwajiri mkuu kwa mujibu wa sheria.
Hiyo ndio hoja kwenye uzi huu? Kama dhalimu magu alikuwa anakemea wazembe kipi kilimfanya amtoe CAG kinyume cha sheria?
 
Huwezi kuelewa hii ni kwa wenye akili timamu tu.
Mwenye timamu ndo utakuwa wewe? Yaani dc amuonee wivu mkurugenzi anayeripoti kwake? Kila kinachofanywa na mkurugenzi lazima dc akijue ila si kila kinachofanywa na dc mkurugenzi lazima akijue sasa hapo wakumuonea wivu mwenzake ni nani?
 
Ndiyo maana nakuambia,hii issue ni kwa wenye akili timamu tu,huwezi kuelewa.

Unarudia kilekile nilichoandika mwanzo ila unaacha kuzungumzia kiini cha hoja yangu!

Nani anakusanya mapato? DC ni mkubwa kimamlaka tu ila ofisi yake ni kapuku.

DED anajinunulia gari analotaka kwa mapato ya halmashauri,vipi DC? Mpaka akumbukwe na TAMISEMI?

Ofisi nyingi za DCs hata magari hawana wanaazima kutoka Halmashauri.
 
DED anajinunulia gari analotaka kwa mapato ya halmashauri,vipi DC? Mpaka akumbukwe na TAMISEMI?
Anaweza kujinunulia gari analotaka kwenye halmashauri yenye madiwani misukule na wilaya yenye dc asiyejitambua!! Dc anayejitambua akizuia mkurugenzi asifuje fedha za halmashauri si kwamba anamwonea wivu mkurugenzi bali anatambua mamlaka na majukumu yake!!
 
Ofisi nyingi za DCs hata magari hawana wanaazima kutoka Halmashauri.
Ofisi ya dc haiwezi kuazima gari bali inaamuru na kuelekeza maybe gari la idara ya utumishi haliko bize liende likafanye kazi tarura kuna operation maalum inataka magari mengi, halmashauri iliyopo chini ya mkurugenzi na taasisi za serikali kuu zilizopo chini ya das elewa kuwa top wao ni dc na anaweza kuamuru na kuelekeza vyovyote anacojisikia.
 
Back
Top Bottom