RC mpya wa Geita ashangaa stendi kuu ya Mkoa kuwa ya matope wakati kuna utajiri wa dhahabu

RC mpya wa Geita ashangaa stendi kuu ya Mkoa kuwa ya matope wakati kuna utajiri wa dhahabu

Tuseme kweli kupitia Fashisti Yule wasukuma mmeonekana ni watu wa hovyo sana.
Mkuu mimi sio msukuma ingawa ni mwenyeji wa kanda ya ziwa.

Simiyu, Geita, Shinyanga, Mwanza na Tabora ni mikoa ya wasukuma ndio kabila kubwa kuliko yote Tanzania.

Usiwaunganishe wote kwa kumtazama mtu mmoja tu.

Kama wasukuma wangekuwa sio waungwana hii nchi siku nyingi ingeshamegwa tangu enzi za JKN.
 
Tunachosahau watanzania ni ukweli kwamba sisi tunapita njia.

Huo uwanja utakuja kutumika siku fursa za maeneo hayo zikifunguka kwa mapana yake....
Kwa nchi masikini Kama hii haingii akilini kutoishi kwa vipaumbele.

Hakuna justification yoyote inayoweza eleweka kuwa chato kulikua umuhimu wa kujengwa Airport ya kiwango kile Kama si ulimbukeni na ubinafsi.

Kwa uchache wa rasilimali isingetarajiwa Leo kuna stendi zenye tope tena za mkoa huku kuna viwanja vya ndege vya kuchezea popo!!
 
Airport zote Tanzania zinakarabatiwa na zote ni muhimu.

Kumbuka ukanda ule ardhi yake ni madini matupu hivyo ni suala la muda tu maendeleo kufika.
 
Mkuu mpya wa mkoa wa Geita mh Rose amesema ameshangazwa sana kukuta mkoa wa Geita una stendi kuu ya mabasi ya matope.

RC Rose amesema stendi ndio reception hivyo hutoa taswira ya mkoa ilivyo kwahiyo ni lazima utajiri wa dhahabu utumike kujenga stendi kuu ya kisasa na siyo hiyo ya kwenye matope.

Rose aliyasema hayo mbele ya wananchi na watendaji alipowasili mkoani Geita tayari kukabidhiwa ofisi.

Source ITV habari!
Ahsante RC Rose kwa kuliona hilo. Ila ujue watu watakukumbusha hii kauli siku za mbeleni kama hautafanya kitu kwenye hiyo stendi wakati wa kipindi chako.
 
Je mkoa wa Geita pia una hospitali kubwa kama ya Rufaa ya Bugando au mkuu wa mkoa wa Geita anataka kujenga kwanza stendi kubwa ya kisasa ya mabasi. Huduma bora za Afya kwa wanaGeita kwa ajili ya kina mama na watoto zipo au kipaumbele ni stendi.

Hospitali ya Bugando mkoa wa Mwanza

Ashawahi fika stendi ya bukoba?

Kusema ukweli viongozi wanazingua sana
FB_IMG_16206789940745754.jpg
 
Mkuu mimi sio msukuma ingawa ni mwenyeji wa kanda ya ziwa.

Simiyu, Geita, Shinyanga, Mwanza na Tabora ni mikoa ya wasukuma ndio kabila kubwa kuliko yote Tanzania.

Usiwaunganishe wote kwa kumtazama mtu mmoja tu.

Kama wasukuma wangekuwa sio waungwana hii nchi siku nyingi ingeshamegwa tangu enzi za JKN.
Mwendazake amewaharibia sana, japo hata kabila lake plus elimu yake vina utata sana
 
Mwendazake amewaharibia sana, japo hata kabila lake plus elimu yake vina utata sana
Kaharibu humu jukwaani huko kwa wananchi wamelia na kuomboleza sana.

Wasukuma wanaonewa kutukanwa, nchi yetu ilikosa nidhamu kabla ya hayati.

Nimezungushwa miaka 29 kupata hati ya ardhi yangu pale wizarani mpaka alipoingia JPM ndio nimeipata.

Matapeli wa wizarani na wale wa mikocheni walikuwa na timu inayodhulumu watu. Hayati alimaliza kabisa upumbavu huo.

Wengi wanaomtukana ni wa humu jukwaani sio wananchi wa kawaida.
 
Mkuu mpya wa mkoa wa Geita Mheshimiwa Rose amesema ameshangazwa sana kukuta mkoa wa Geita una stendi kuu ya mabasi ya matope.

RC Rose amesema stendi ndio reception hivyo hutoa taswira ya mkoa ilivyo kwahiyo ni lazima utajiri wa dhahabu utumike kujenga stendi kuu ya kisasa na siyo hiyo ya kwenye matope.

Rose aliyasema hayo mbele ya wananchi na watendaji alipowasili mkoani Geita tayari kukabidhiwa ofisi.

Chanzo: ITV habari!
Angeshangaa Watanzania kuwa MASIKINI Miaka 60 ya UHURU Nchi ina RASLIMALI LUKUKI
 
Back
Top Bottom