RC mpya wa Geita ashangaa stendi kuu ya Mkoa kuwa ya matope wakati kuna utajiri wa dhahabu

Geita wameniangusha sana!
 
Philipo Linda heshima yako JF kwa kuacha Kutetea Mambo ya hovyo
 
ni 5 Tena kwa msukuma na CCM
 
umeongea kitu cha maana sana!! wengi ya waafrika tunaangalia kesho yake tu!! Hatuangalii wakati ujao!! Huo uwanja wa ndege utakuja kutufaa baadae fursa za mikoa hiyo ikifunguka!!
 
Vyote ulivyotaja vinatengewa pesa siku zote.
Unafahamu kwamba uwanja huo haujawahi kupangiwa budget?, haujawahi kupitishwa na bunge? Unafahamu budget hupangwa kwa kufuata umuhimu (vipaumbele - priorities)? Kama maeneo muhimu ya elimu, afya nk, hayajatengemaa, kuna kipaumbele chochote kujenga uwanja wa ndege wenye hadhi ya "International airport" hapo Chato na kuuacha uje uwafae wajukuu wetu miaka 50 ijayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule mbunge wa darasa lasaba msukuma anatokea wapi,Au walikubaliana wajenge uwanja wandege wa chato harafu ndipo ctendi ijengwe
 
Watanzania wanavyokomaaga na vitu vya kijinga utadhani vinawasaidia wananchi.

Ma vitu kama stendi sijui masoko yanasaidia vipi mtu wa kawaida? Maana kutumia hizo huduma lazima kulipia.

Mbona hamshangazwi na watoto kukaa chini,kurundikana madarasani kutokuwa na vyoo vya kutosha,maji,huduma za afya na barabara? Ila stendi ndio imemshangaza? Ajabu kweli kweli
 
Uliujenga wa nini sasa,basi jengeni kila sehemu Ili uendelee kusubiria fursa kufunguka.

Ukute na wewe ni graduate [emoji2][emoji2][emoji2][emoji1]
 
umeongea kitu cha maana sana!! wengi ya waafrika tunaangalia kesho yake tu!! Hatuangalii wakati ujao!! Huo uwanja wa ndege utakuja kutufaa baadae fursa za mikoa hiyo ikifunguka!!
Na vipi thamani ya pesa kwa kuilaza hapo kwa muda wote huo badala ya kuipeleka ikatatue matatizo ya vipaumbele kwa sasa? Pia uwanja na facilities zingine zilizojengwa hapo, baada ya muda mrefu zitahitaji matengenezo (depreciation iko pale pale) kwenye kitu kisichotumika kwa wakati huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama ni vya kijinga lakin stendi kufikia hatua hii kama ya bukoba huu ni upumbavu wa viongozi
 
huyu mama ache upumbavu, yaani mfukoni anazo bili25 za CSR anazo pata kila mwaka kutoka mgodi wa ggm alafu analalamikia matope kwenye stendi ya mkoa wake??? kama ana uchungu kweli na huo mkoa kwanini asitoe mil300 tuu kwenye hizo bilion 25 na kuweka paving blocks apo stendi badala ya kujilipa hizo hela maposho ya vikao hewa na kujinunuliaa ma v8 adi wanatumbuliwa
 
Mwen’zake alikuwa mbinafsi mno kujenga uwanja wa kimataifa kijijini kwake ilhali mkoani stend ni ya matope.
 
Mimi nafikiri shida inaanzia kwenye vipaumbele ( first things first). Unaanzaje kujenga stendi (uwanja) ya ndege kabla ya stendi ya magari, hali ukijua asilimia kubwa ya wananchi wa eneo husika wanatumia usafiri wa barabara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…