RC mpya wa Geita ashangaa stendi kuu ya Mkoa kuwa ya matope wakati kuna utajiri wa dhahabu

Hapo hapo chato kwa walima furu kuna uwanja wa ndege wa kuchezea bata na mwewe.

Hii nchi ilikua kwenye full fascism
Acha dharau ata Geita ni Tanzania pia tujifunze ata kwa wakenya wanavyopendana na wanavyopenda maeneo ya nchi yao.
 
Yaani uache kujenga miundombinu yenye manufaa kwa sasa ujenge miundombinu kwa ajili ya kizazi kijacho, je umeshafikia mahitaji ya kizazi cha sasa? Mfano ndio huo wa stendi tope.
 
Mimi nafikiri shida inaanzia kwenye vipaumbele ( first things first). Unaanzaje kujenga stendi (uwanja) ya ndege kabla ya stendi ya magari, hali ukijua asilimia kubwa ya wananchi wa eneo husika wanatumia usafiri wa barabara?
Uwanja wa ndege na stendi vyote viwili vinaweza kujengwa sambamba. Mpanda ndege anaweza akawa ni mgeni kutoka nje na stendi ikajengwa kwa ajili ya abiria wa eneo husika.

Vyote viwili ni vichocheo vya maendeleo, inategemea na mtazamo wa mtu mmoja mmoja.
 
Yaani uache kujenga miundombinu yenye manufaa kwa sasa ujenge miundombinu kwa ajili ya kizazi kijacho, je umeshafikia mahitaji ya kizazi cha sasa? Mfano ndio huo wa stendi tope.
Mkuu viwanja vya ndege vinaifungua nchi kimataifa wakati stendi zinaifungua nchi kwa ajili ya abiria wa ndani. Vyote viwili ni muhimu kuwepo, ndege sio anasa kama tunavyojaribu kudanganyana tunapokuwa kwenye mijadala yetu.
 
Mkuu viwanja vya ndege vinaifungua nchi kimataifa wakati stendi zinaifungua nchi kwa ajili ya abiria wa ndani. Vyote viwili ni muhimu kuwepo, ndege sio anasa kama tunavyojaribu kudanganyana tunapokuwa kwenye mijadala yetu.
Kama hakuna stendi mabasi ya kuifungua nchi hayaji au?
 
Zile mbwembwe za musukuma kumbe stendi yake ni tope tupu kama Bukoba!!
Mnyonge mnyongeni Mkuu lakini haki yake apate..Alipinga mno ufisadi uliofanyika pale lakini wapi...almanusura avue gamba na avae gwanda enzi Zile...ikawa apokwe tena kadi ya CCM na wao...mara akatwe...nk.Acha kabisa CCM inawenyewe,...mwisho akaulizwa ni Ubunge Wa Geita mjini tu au!?.Basi tunaligawa kutakuwa na Jimbo la Geita Vijijini,nenda huko..akatulia.!Hupiga kampeni bila sapoti ya Chama Chake huko...Acha kabisa
 
Halafu hapo si yule mkurugenzi alininua v8 ya 460ml
 
CHADEMA walikuwa wanongoza hii nchi, wameshindwa hata kujenga stendi ya chngarawe achilia mbali lami.

Hii nchi bhana, alafu CHADEMA wakaenda kujenga uwanja wa ndege huko porini CHATO na mbuga ya Burigi badala ya kuanza na maendeleo ya stendi ili wapate kodi.

"mwendazake"
 
Nadhani mikoa ya kanda ya ziwa imelaaniwa... Shinyanga pekee ndio ina lami labda kidogo na Bariadi aka Simiyu hiyo mi-Mwanza, Kagera, Mara, Geita... vumbi mpaka....
 
Sababu ni kutumiwa na mabeberu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…