RC Mtaka aomba radhi baada ya kuwaambia wananchi wampuuze Waziri Ndalichako

RC Mtaka aomba radhi baada ya kuwaambia wananchi wampuuze Waziri Ndalichako

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram:

"Nimesoma na kupokea maoni,ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile naomba Radhi kwa wote waliokwazika ,wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno "Waziri" lilipobeba hisia tofauti nawaheshimu Mawaziri wote na nafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa natambua pia kazi nzuri inayofanywa na Mawaziri wetu wanaosimamia sekta ya elimu - Wapo wanaodhani maelezo ya hisia zangu ni kuanza kupandisha mabega,na pengine mgema akisifiwa tembo hutia maji-niwaondoe hofu sina sababu ya kupandisha mabega ."

E6LzFwIXEAEua5e.jpg
 
Gender Gender !!

18 nje ya box....kwaa mbalii mtu anapiga jaramba
 
Huyu ni wa kutumbuliwa tu, mbona vijana wenye uwezo zaidi yake kuweza kuongoza mkoa wako wengi sana!
 
Kabisa KATIBA MPYAA haiepukiki

Mgambo watazidi kukanyagana huu mhula...
 
Sasa mh Mtaka ameniangusha, anaomba radhi, mbona sion shida amesema ukweli na ukweli humuweka mtu huru
 
Namshauri RC Mtaka arudi eneo alipotenda kosa aombe radhi mbele ya wananchi aliowaambia wampuuze Waziri wa Elimu.
 
Elimu msingi na sekondari ni bora zikapelekwa wizara ya Elimu na zikawa chini ya idara maalumu za kuzisimamia, elimu msingi na sekondari kuwa chini ya TAMISEMI ni hatari maana linachezewa sana na wanasiasa
 
Hata kama alikuwa na pointi kwenye ujumbe wake lakini uwasilishaji wake wa huo ujumbe ulikuwa wa kitoto sana, ile mihemko sijui aliitoa wapi,

Hakuwa na sababu ya kurudia mara mbili ile kauli kisa amevaa barakoa, ameonesha kama alikuwa na chuki binafsi na waziri, au alitaka sifa za kijinga mitandaoni.

Ndalichako kwa mtazamo wangu angejiuzulu kulinda hadhi yake, ile mihemko ya Mtaka itamuweka kwenye wakati mgumu mbele ya safari akitimiza majukumu yake.

Na Samia asipokuwa mkali kuwanyoosha hawa vijana, iko siku watendaji kwenye serikali yake watatukanana hadharani wakitafuta sifa kwa wananchi mitandaoni.
 
Ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram:

"Nimesoma na kupokea maoni,ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile naomba Radhi kwa wote waliokwazika ,wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno "Waziri" lilipobeba hisia tofauti nawaheshimu Mawaziri wote na nafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa natambua pia kazi nzuri inayofanywa na Mawaziri wetu wanaosimamia sekta ya elimu - Wapo wanaodhani maelezo ya hisia zangu ni kuanza kupandisha mabega,na pengine mgema akisifiwa tembo hutia maji-niwaondoe hofu sina sababu ya kupandisha mabega ."

View attachment 1851748
Kuomba radhi ni uungwana pale mtu anapobaini amefanya kosa/makosa

Hongera zake kwa kuomba radhi maisha yasonge mbele.
 
Back
Top Bottom