Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amekana kuhusika na tukio la ukamataji viongozi na wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mwanza leo wakielekea ofisini kwake.
Asubuhi ya saa 3:30 kuelekea saa 4 kamili viongozi na wanachama wa chama hicho wakiongozwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Zakaria Obad walipokuwa wamekaribia kufika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kwenda kufuatilia tukio la kiongozi wao kutekwa, wanadai kukamatwa na Jeshi la Polisi ambao waliwataka kwenda kituoni kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Soma, Pia: Makada 20 wa CHADEMA wakamatwa wakielekea kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza kufuatilia mwenzao aliyepotea kwa siku 12
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa baadhi ya viongozi wa Chama hicho wamedai mbali na kukamatwa bila sababu za msingi pia baadhi yao wamepigwa wakati wakijaribu kuhoji wakiwa kituo cha polisi.
Hata hivyo wamedai mbali na kuwaeleza maofisa hao kuwa wana ahadi ya kukutana na RC Mtanda bado waliendelea kushikiliwa pasipo kupewa nafasi ya kujieleza huku wakijibiwa kuwa hawana taarifa hiyo.
Hata hivyo Mtanda amekana kuhusika na ukamataji huo huku akidai alikuwa na ahadi ya kukutana nao na asingeweza kufanya kitendo hicho na kuongeza kuwa wakati wowote CHADEMA wanakaribishwa kwenye ofisi yake.