RC Mtanda: Naviachia Vyombo vya Usalama kuchunguza kama nilihusika kwa namna yoyote kwenye tuhuma za ulawiti zinazomkabili Dkt. Nawanda

Mkuu wa mkoa wa Mwanza mh Mtanda amesema amekuwa na uvumilivu mkubwa kwa Maneno yanayoongelewa mitandaoni yakimuhusisha na tuhuma za Dr Nawanda

Mtanda amesema amemsikia Tusiime akimuhusisha kwa namna fulani kwenye swala hilo lakini yeye anaviachia Vyombo vya Usalama kuchunguza kama alihusika kwa namna yoyote ile

Source: Mwananchi
Walawiti wanajuana na wanateteana vibaya sana, tena wanapendana mno. Wakimsikia mwenzao mmoja makubwa yememfika, utawaona jinsi wanavyotoka hadharani kumtetea. Mungu anawaona nyie ibilisi wakubwa waharibifu wa matundu ya watoto wa watu.
 
Vyombo gani vya usalama wakati yeye amehusika kuvisuppress visifanye kazi yake??? amejaza mapete vidoleni utadhani mpunga majini, yaani tiss salamu zao! Mungu atulipie kisasi kwa mabaya wanayotutendea watanzania.
Shetanii ni kiumbe cha hovyo sana.
SHETANI NI MShenzi sana .
 
Kwa nchi zinazoendelewa kwa manufaa ya heshima yake na kwa manufaa ya public interest huyo RC alitakiwa ajiuzulu. Huwezi kufanyiwa uchunguzi ukiwa bado RC unaleta conflict of Interest. Sijui kwanini hawapendi kujiuzulu
Njaa mbaya sana 📌📌📌
 
MTANDA anadai kutohusika na jambo lolote juu ya binti aliyelawitiwa lakini ajue vyombo vya uchunguzi kama vinataka kumuweka wazi kwa maneno aliyoyasema na wanahabari kwamba hakuwahi kuwasiliana na TUMSIME je endapo namba yake itabainika ilikuwemo kwenye mawasiliano ya binti huyo kwa tarehe tajwa atafanya nini!

Mtu kama MTANDA unasema uongo kwa binti yako wa miaka 21 uonekane mwema kwenye jamii! Hivi uongozi mlionao mpo kwa ajiri ya kuharibu kizazi cha watu wenye kipato cha chini, ! Nilitegemea utubu dhambi zako kwani hayo unayojaribu kukwepa uliyafanya mbele ya Askari wa mwanza na taarifa zako zipo Leo hii unaongea kwa kujiamini kisa umekuwa kiongozi ukiwa na miaka 17 kwani kusema hivyo ndiyo unaonekana mwadilifu! Hutambui kuwa kuna watu wanakua hadi uzeeni NI wajinga ! Hivyo viti mnavyokalia viheshimuni kwa kusaidia watu wenye shida siyo kukandamiza watu ambao hawapo kwenye mfumo.

Binafsi nasema NI aibu kuwa na kiongozi Aina ya RC MTANDA unatoka hadharani huku unatoa zawadi kwa Askari polisi waliofanya vizuri kwenye sherehe yao unasema vyombo vichunguze wewe kama umehusika kufifisha kesi ya binti huyo huku vyombo hivyo vya uchunguzi viko chini yako ndani ya mkoa kwanini usijiuzuru ukavipa mwanya wakafanya kazi hiyo.
 
Mmh Hilo suala litaenda mbali Sanaa na mwisho wake RC kama amehusika itakuwa haileti maana ya uongozi, ni jambo la kufatiliwa kabisa
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameibuka, baada ya Tumsime Ngemela kumtaja alipozungumzia tuhuma za kulawitiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda.

Tumsime akizungumza na waandishi wa habari jana Julai 5, 2024 jijini Dar es Salaam, alimtuhumu Mtanda kwamba alimshawishi kufuta malalamiko aliyoyafikisha polisi dhidi ya Dk Nawanda.

Mtanda amesema anaviachia vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza tuhuma za yeye kuhusika kwenye sakata hilo.

Mtanda leo Julai 6, 2024 wakati wa hafla ya kutoa zawadi na sifa kwa wakaguzi na askari polisi waliofanya vizuri mwaka 2024, amesema amekuwa na ustahamilivu baada ya kusikia watu wakimsema vibaya mtandaoni.

Huku, akitaja 4R za Rais Samia Suluhu Hassan, Mtanda amesema yeye ni mstahamilivu wa kisiasa hana haja ya kujibu mtu yeyote kwa kuwa anajua tayari vyombo vya usalama vinafanya kazi yake.

“R ya pili resilience (ustahimilivu) wa kisiasa na hata sisi viongozi lazima tuwe wasitahamilivu… jana nilikuwa naona kwenye mitandao watu wanasema maneno ya ajabu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza lelelelelele…

“Lakini kwa sababu mimi ni mstahamilivu wa kisiasa sina haja ya kujibu mtu yeyote ninachojua vyombo vya kisheria vinafanya kazi yake, Jeshi la Polisi lakini pia mamlaka nyingine zinaendelea na uchunguzi na kuingilia chunguzi hizo ni kuingilia misingi ya utawala bora,” amesema Mtanda.

Ametaka vyombo hivyo vya kiuchunguzi viachwe vitimize wajibu wake bila kuingiliwa ili visichelewe na kukwamishwa kutimiza wajibu wake.

“Hii ni kitu ambayo inaitwa ustahimilivu na sisi viongozi lazima tuwe hivyo, kiongozi wa kisiasa lazima awe na ngozi ngumu siyo unaguswa kidogo unaanza kulialia. Nimekuwa kiongozi nikiwa na miaka 17 nikiwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya leo nina umri mkubwa nimekuwa na experience (uzoefu) ya kutosha kwa hiyo ninao uvumilivu katika masuala ya uongozi na utawala bora,” amesema.

Akizungumza na wanahabari akiwa ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Tumsime alidai alipigiwa simu na Mtanda aliyemweleza anahitaji kuonana naye, akamweleza kwamba yupo na polisi.

“Akasema wape simu akaongea nao na kuniamuru wanipeleke ofisini kwake. Tulipofika akawaambia polisi watoke nje, ili tuzungumze wawili, akaniambia kesho nikaifute kesi,” alidai Tumsime.

Alidai baada ya kuzungumza naye aliwaita askari polisi wakaingia ndani na akawaeleza makubaliano yamefikiwa ya kufutwa kesi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, Jeshi hilo Julai 5, 2024 lilipokea taarifa za uchunguzi wa vielelezo kuhusu madai ya Dk Nawanda kumlawiti binti huyo, kutoka maabara za uchunguzi wa kisayansi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Juni 2, 2024 saa moja usiku katika eneo la maegesho la moja ya baa mashuhuri jijini Mwanza.

Alidai aliingiliwa kwa nguvu kinyume cha maumbile kwenye gari dogo linalomilikiwa na mtuhumiwa.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma
- RC Said Mtanda wa Mwanza hastahili kuwa kiongozi wa umma kwa kutaka kuzima kesi ya Binti Tumsiime anayedai kulawitiwa na Dkt. Nawanda
Ajiuzuru kwanza vyombo vya dola viwe huru!
 
Akae pembeni wakati wa uchunguzi. Anataka vyombo vimchunguze wakati yeye ndio anavisimamia!
 
Anasema hivyo kwa sababu anajua hakuna uchunguzi wowote unaoendelea! Mke wa Kaisari hastahili hata kushukiwa kuwa ni msinzi! Kiongozi wa serikali mkubwa kushiriki kuficha jinai ni kosa kubwa sana! Na ikumbukwe kuwa wawili hawa ni ndugu!
 
Uzuri wengine tunakufahamu vizuri wala hutudanganyi.
 
Halafu dogo anamwita kwa jina moja tu Nawanda.

Hapo ameshamdharau na kumuona kama msela fulani hivi kumbe mteule wa Rais.

Haya majamaa yanamuaibisha sana Rais aliyewateua.
 
Hebu tuwekeeni vifungu vya sheria.

Mbona mashoga hawakamatwi?

Kama kuna sheria kama hiyo, basi ni ya kipuuzi. Unawekaje sheria kwa kitu ambacho mtu anakifanya wakati wamapenzi akiwa amejificha chumbani?
Kifungu cha 154 cha kanuni za adhabu ama penal code inakataza un natural offence.
 
Kiongozi ni kioo cha jamii.lakini zama hizi imekuwa kinyume kabisaa!!!
hatuna viongozi waadilifu!!!! Uhuni uzinzi, usaliti ndio umeshamiri maofisini.
 
Back
Top Bottom