RC Mtanda: Suala la dampo katika makazi ya watu Kata ya Usagara, litashughulikiwa na DC na Halmashauri ya Misungwi

RC Mtanda: Suala la dampo katika makazi ya watu Kata ya Usagara, litashughulikiwa na DC na Halmashauri ya Misungwi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baada ya Mdau aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Usagara A, Kata ya Usagara, Wilayani Misungwi kueleza kuwa licha ya kutozwa fedha kwa ajili ya uzoaji taka lakini wamewekewa dampo la taka kwenye makazi yao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ametoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.

Hoja ilivyokuwa ~ Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi tumewekewa dampo kwenye makazi ya watu

RC Mtanda amesema “Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ataifanyia kazi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Misungwi kuondoa kero hii, Thank you for your attention to the matter.”

Baada ya maelezo hayo Mwananchi mmoja kupitia ukurasa wa Instagram akamuuliza, Nyie kufanya kazi kwenu hadi Wananchi walie mtandaoni?”

Mtanda akamjibu “Sio lazima, yapo mengi tunayoyafanya bila kuyaona kwenye mtandao ambayo wewe huyafuatilii kwa sababu huna hobi nayo, lakini hii ni platform pia ya kusikia yaliyopo katika umma na tukiyaona tunayafanyia kazi. Mkoa una watu milioni 3.6, wilaya 7 utajua yote? Mengine utasikia, mengine kuyaona, mengine kuyasoma. Thanks for under standing👏👏”

Pian soma ~ DC Johari Samizi: Dampo lililokuwa katika makazi ya watu Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi limeondolewa
 
Mtanda ni mzito sana wa fikra kama mwili wake ulivyomzito mzito...anapitwa kushoto na mambo mengi anakuja kuyajulia Mtandaoni huku.

Nina mashaka sana na kiwango chake Cha Mahusiano Kazini... Hapo amejikosha tu ila atafakari kwa kina hilo swali la huyo Mwananchi.
 
Back
Top Bottom