DOKEZO RC na RPC Dodoma, Polisi Jamii Kata ya Nala anatunyanyasa sana, tafadhali muondoeni

DOKEZO RC na RPC Dodoma, Polisi Jamii Kata ya Nala anatunyanyasa sana, tafadhali muondoeni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Weka namba zake za simu hapa .
Pia kama umewahi soma majina yake yote na namba ya kazi kwenye uniform zake weka hapa .
Pole sana ila siku nyingine jisimamie usiwe mnyonge hivyo ndugu yangu
 
Wanaume wa dodoma mna taka kua kama wa dar sasa wana ogopa mbwa 10...yani mvuta bangi mmoja mna muandikia uzi
Dar hakuna upuz huo
Huyo angeshashugulikiwa
Kitambo tu

Ova
 
Yaani askari jamii anawasumbueni na nyie
Mmekaa tu

Ova
 
Naandika kwa uchungu mkubwa baada ya Mke wangu kufanyiwa udhalilishaji na huyu kijana mhuni anayeitwa MALIMA ambaye ni Polisi Jamii hapa Kata ya Nala.

Ni kijana ambaye anajiona yeye ni zaidi ya Polisi wa kawaida. Yeye ndie Polisi,yeye ndie Mwanasheria,yeye ndie Hakimu,yeye ndie Magereza. Kazi yake ni kukamata watu na kuwalazimisha wampe pesa akidai ili asiwafikishe Kituo cha Polisi.

Nimesikia Dodoma ameletwa RPC mpya ambaye ni Mwanamama hivyo RPC na RC wote ni wakinamama.

Tafadhali njooni Kata ya Nala itisheni kikao cha wananchi ili tuwaambie malalamiko yetu dhidi ya huyu Polisi Jamii anayeitwa MALIMA.

Ni mnyanyasaji sana kwa Wananchi wanyonge hasa wanawake kwa kuwa hawajui Sheria na Haki zao za msingi.

Haiwezekani mtu mmoja mhuni tu kwa kofia ya upolisi jamii awasumbue wake zetu kwa kumwaga vyakula vyao vya biashara akisema wamechafua mazingira kwa kumwaga maji yenye ukoko wakati ukweli ni kwamba aliwatongoza wakamkataa, na sasa anawakomesha kwa kuwakamata na kutaka wampe pesa akitishia kuwafunga jela.

Diwani anazo taarifa za unyanyasaji unaofanywa na huyu kijana lakini amekaa kimya. Tafadhali RC na RPC mpya Dodoma njooni Nala, itisheni Kikao ili msikie malalamiko yetu dhidi ya huyu mhuni polisi jamii anayeitwa Malima, tafadhali tusaidieni tumechoka na manyanyaso na uonezi wake.
Kaka umeshindwa hata kununua manati umlenge usku uone kama atarudia ujinga ule ,

Tafuta manati au yai Visa mlenge nayo hata rudiaaa ujinga ule
 
Weka namba zake za simu hapa .
Pia kama umewahi soma majina yake yote na namba ya kazi kwenye uniform zake weka hapa .
Pole sana ila siku nyingine jisimamie usiwe mnyonge hivyo ndugu yangu
Ndugu,uwezo wa kupambana nae kwa ngumi ninao,tatizo watu wanatembea na magonjwa yao,naweza kwa hasira nikamtwanga ngumi akadondoka akanifia,kwa umri wangu kuanza kuburuzwa Mahakamani kwa Mauaji nitafia hukohuko
 
Inashangaza pia Mpo Nala.
Namba ya DC hamuna
Namba ya OCD hamna
Namba ya RC hamna
Namba ya DAS au RAS hamna
Namba ya RPC hamna
Namba ya RCO hamna
Namba ya Mnadhimu wa Polisi pia hamna?
😀

Ni uzembe pia huu
Mnachanganya kati ya Askari Ofisa wa Polisi na Polisi Jamii (PJ-Askari wa ulinzi shirikishi AUXILIARY POLICE).

Huyu anayelalamikiwa ni Polisi Jamii (Same to mgambo wa jiji)
 
Weka namba zake za simu hapa .
Pia kama umewahi soma majina yake yote na namba ya kazi kwenye uniform zake weka hapa .
Pole sana ila siku nyingine jisimamie usiwe mnyonge hivyo ndugu yangu
Polisi jamii hawana namba wala majina wale ni mgambo waliozubaa, wanawajibika kwa Mkurugenzi
 
Polisi jamii hawana namba wala majina wale ni mgambo waliozubaa, wanawajibika kwa Mkurugenzi
Ndugu nitakuwa sikumuelewa maana nilijua ni wale askari kata hivyo ndiyo maana nikataka namba yake ya kazi .
Kama ni hao wajinga katafute ukapige vichwa tu
 
Uko Dodoma makao makuu ya nchi takatifu ya Tanzania unatishwa na mgambo aliyejibatiza jina la polisi jamii?

Alipaswa kuwa ana nyuzi 10 kichwani huyo mhuni wenu.

Mtumue IGP wambura SMS kwenye na 0699998899

Andika jina lako, mkoa, wilaya, tarafa, kata, namba ya simu ili iwe rahisi Kwa timu ya makachelo wanaofoadiana sms kuchukua hatua
 
Mnachanganya kati ya Askari Ofisa wa Polisi na Polisi Jamii (PJ-Askari wa ulinzi shirikishi AUXILIARY POLICE).

Huyu anayelalamikiwa ni Polisi Jamii (Same to mgambo wa jiji)
Ni kweli,ni kimgambo fulani kipuuzi sana na Raia kwa kutokujua haki zao wanakubali kuonewa sana
 
Ni kweli,ni kimgambo fulani kipuuzi sana na Raia kwa kutokujua haki zao wanakubali kuonewa sana
Sasa watu wanachanganya huyo Polisi Jamii (AUXILIARY Police) na Askari Polisi (Police officer)
 
Mkuu huyo mpuuzi mmoja ndio anakufanya uanzishe uzi? Hebu mvizie usiku uchochoroni, uyamalize nae mkiwa wawili tu bila ushuhuda wa walimwengu, kuna nyakati inabidi uchukue hatua stahiki kulinda heshima yako na mkeo.
 
Nimeanza kwa kutoa taarifa ili viongozi wachukue hatua,zaidi ya hapo Wananchi tutajichukua Sheria mkononi
 
Wanaume sijui tumekuwaje siku hizi, baada upambane kiume na huyo Malima anayemzingua mke wako, unakuja kuweka JF, itakusaidia nini sasa maana ni mpaka waone na wanaweza wasione pia au waone na wapotezee.
 
Nimeanza kwa kutoa taarifa ili viongozi wachukue hatua,zaidi ya hapo Wananchi tutajichukua Sheria mkononi
Usiongelee haya mambo kwa wingi, kama mke wako kazinguliwa, hii ni issue yako binafsi mkuu. Wanaume siku hizi tumekuja kuwaje jamani..?
 
makonda aliisha wambieni mnamatatizo nendeni ofisi za chama wakishindwa nendeni makao makuu mkamuone hata hili nalo mnashindwa
 
Ndugu,uwezo wa kupambana nae kwa ngumi ninao,tatizo watu wanatembea na magonjwa yao,naweza kwa hasira nikamtwanga ngumi akadondoka akanifia,kwa umri wangu kuanza kuburuzwa Mahakamani kwa Mauaji nitafia hukohuko
Weka namba zake mkuu , sjue amemulikwa
 
Mnachanganya kati ya Askari Ofisa wa Polisi na Polisi Jamii (PJ-Askari wa ulinzi shirikishi AUXILIARY POLICE).

Huyu anayelalamikiwa ni Polisi Jamii (Same to mgambo wa jiji)
Kaka Police Jamii ni Idara ndani Jeshi la Polisi.

Je mtoa mada atuambie huyu mlalamikiwa ni Askari wa idara hiyo ama ni wale Ulinzi Shirikishi (Sungusungu) ?
 
Polisi jamii hawana namba wala majina wale ni mgambo waliozubaa, wanawajibika kwa Mkurugenzi
Mnachanganya.

Polisi jamii ni idara ndano ya jeshi la polisi.

Mgambo wa mkurugenzi hawaingii hapo ktk category ya PJ
 
Back
Top Bottom