DOKEZO RC na RPC Dodoma, Polisi Jamii Kata ya Nala anatunyanyasa sana, tafadhali muondoeni

DOKEZO RC na RPC Dodoma, Polisi Jamii Kata ya Nala anatunyanyasa sana, tafadhali muondoeni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Polisi Jamii ni Mgambo tu hawezi kuwa Askari wa Jeshi la Polisi. Ni mgambo kama migambo wengine tu.
 
Hatimaye nimepewa taarifa muda huu kumeitishwa kikao pale jamaica watu wanafunguka.
 
Kaka Police Jamii ni Idara ndani Jeshi la Polisi.

Je mtoa mada atuambie huyu mlalamikiwa ni Askari wa idara hiyo ama ni wale Ulinzi Shirikishi (Sungusungu) ?
MREJESHO:Huyo Malima ni MGAMBO(lakini kwa kuwa jina la Mgambo hawalipendi)huwa wanajiita Polisi Jamii au Ulinzi Shirikishi.
Mrejesho ni kwamba Uzi huu ulisomwa na Maofisa wa Polisi Makao Makuu na leo walikuja na kuitisha Kikao kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa Nala na Wananchi wakafunguka mabaya ya huyo Mhuni Mgambo Malima.
Imeamriwa AACHE kufanya shughuli hizo kuanzia leo kwa muda wa miezi mitatu wakati uchunguzi wa Jinai zaidi unafanyika dhidi yake. Imekuwa ni furaha kwa wananchi wengi walioonewa na huyo mhuni kwa kisingizio cha Polisi Jamii wakati ni MGAMBO kama MIGAMBO wengine tu
Asante Jamii Forum
 
Nala ya kwanza mpaka Jamaica ndio maeneo yake,yaani Wake zetu wakimuona anapita hujifungia ndani kwa jinsi alivyo mnyanyasaji,Nchi imekuwa na mambo ya ajabu sana hii. Diwani yupo na anajua,Mtendaji wa Mtaa yupo na anajua lakini wanafumbia macho hali hii
Kamateni huyo kibaka mumchome moto kama vibaka wengine tu.
 
Kaka Police Jamii ni Idara ndani Jeshi la Polisi.

Je mtoa mada atuambie huyu mlalamikiwa ni Askari wa idara hiyo ama ni wale Ulinzi Shirikishi (Sungusungu) ?
Hiyo 'idara' ndo umeiweka wewe?

Hujui hata neno IDARA lina maana gani.
Unataka kuzungumzia kamisheni ya Community engagement (USHIRIKISHWAJI JAMII) Community Policing na kuichanganya na AUXILIARY Police, vitu viwili tofauti we usiyejua.
Sasa kama mtoa thread mwanadodoma ameshasema ni walinzi wa auxiliary police ww ni nani utuchanganyie madesa kutuletea upopoma wako vitu vyenyewe huvijui, eti ndani ya polisi kuna idara, teh teh teh, rudi shule
 
Namfahamu huyo anayelalamikiwa Malima. Ni mpuuzi mmoja ambaye hata mimi alishawahi kunikuta napata bia zangu saa 5 Pub akaanza kunihoji eti kwa nini nakunywa Pombe muda wa kazi. Bila kuamuliwa na watu waliokuwa jirani ilikuwa nimng'oe meno. Ni kijamaa kipumbavu kinachoonea sana wananchi wasiojitambua hasa Wanawake. Anachokifanya huwa anachukua mfano TV yake au Subwoofer halafu anampa kijana anayefahamiana nae kisha anamwambia katafute Mteja hasa kwa vijana wenye viduka na vibiashara kule Nala. Kijana anaenda anauza huo mzigo. Kisha baada ya saa 1 huyu Malima anaenda na yule kijana aliyeenda kuuza akiwa amemfunga pingu mpaka pale alipouza. Anaanza kumtisha yule mnunuzi kwamba amenunua kitu cha Wizi na yupo chini ya ulinzi. Mnunuzi unakuta kweli mzigo bado upon palepale dukani kwake hivyo lazima aogope. Hivyo huyu Polisi Jamii anampiga Mnunuzi Mkwara inabidi mnunuzi akubali kuachia alichonunua kwa Malima bila kurudishiwa pesa yake. Malima anabeba mzigo wake anaurudisha kwake,kisha anarudi tena kwa mnunuzi kumtisha atoe pesa ili Kesi ifutwe kituoni. Kwa kuwa mnunuzi ni mshamba na muoga inabidi atoe pesa nyingine na kumpa huyo Malima bila kujua suala lote lilikuwa ni mpango.
Hivyo ni kijamaa kipumbavu sana sana
Loooo!! Nimeumia sana kwamba ,wezi wa namna hii bado wapo na wanaendelea kutesa watu tena kwa kofia ya taasisi za serikali
 
Kama mhuni,si na nyie mfanyieni uhuni.
Kwani anaishi kota za Polisi kusema kwamba anakuja huko Kwa usafiri na anarudi Kwa usafiri na Dereva wake.

Dawa ndogo Sana,kifinyo tu.RPC ana kazi nyingi mhurumieni.
Msiwe makondoo kiasi hicho.akikuzingulia familia mzingue na wewe ili ajifunze.
Vizia kamata kata kiganja Cha mkono wa kulia au piga wembe za uso afu mwacheni ajiuguze miezi 6.
Afu mtaona matokeo.

Msipotezeane mda,mda ni Mali.
 
Watanzania uzezeta umezidi, ukondoo wa kipuuzi sana huu,Kenya huwezu sikia malalamiko kama haya, hao Police jamii ingekuwa ni kenya wangekuwa futi 6 chini ya aridhi. Ukondooo umewazidi
Sasa Mkuu kosa la kuombwa Rushwa ya Ngono ni Kifo kweli?

Nchi itatawalikaje?

Kama huyo Polisi Jamii anawataka kimapenzi Wake za Watu ili asiwafikishe Kituo cha Polisi hiyo ni Rushwa kama rushwa zingine mkiona hamsikilizwi mnamuwekea mtego anajaa kwenye Ugoni anakuwa hana ujanja.
 
Back
Top Bottom