Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Serikali imezindua na kukabidhi boti maalum ya uokoaji na kuzima moto yenye thamani ya Sh bilioni 1.5, ikiwa ni hatua ya kuongeza uwezo wa kukabiliana na majanga katika Ziwa Nyasa.
Boti hiyo ina injini mbili zenye nguvu ya Horse Power 250 kila moja, uwezo unaolenga kuimarisha kasi na ufanisi wa operesheni za uokoaji na uzimaji moto majini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika mjini Mbambabay,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amesema uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma muhimu, ikiwemo usafiri wa majini na mifumo ya kukabiliana na majanga.
Amewataka wananchi kuongeza tahadhari wanaposafiri majini, kutumia vifaa vya kujikinga na kuzingatia taarifa za wataalamu wa hali ya hewa.
Soma Pia: RC Ruvuma azindua Coaster jipya lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 334
Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ruvuma, SSF Merania Nyabwinyo, ameishukuru Serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa boti hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa.