Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amemwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Simanjiro kumkamata na kumweka ndani Afisa wa Polisi Kata ya Loibosiriet, Ester Tairo, kwa uzembe kutokana na kushindwa kumkamata kijana aliyemsababishia ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibosho.
Agizo hilo amelitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mama wa binti huyo, Saroni, ambaye anadai kuwa binti yake anateseka kwa kupewa ujauzito na familia ya mwalimu aliyemlea.
Na kwamba hata alipofikisha malalamiko kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Polisi wa Kata, kuhusu mtuhumiwa wa kumpa mimba mwanafunzi, hakuchukuliwa hatua yoyote.