Mkuu wa Mkoa wa Manyara (RC), Queen Sendiga amewakaribisha rasmi wanafunzi 110 wanaoanza kidato cha tano katika Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana Manyara iliyopo mjini Babati.
Katika ukaribisho huo DC Sendiga amevaa sare za shule kama wavaavyo wanafunzi hao kwa lengo la kuwapa morali ya kusoma.
Sendiga amewakaribisha rasmi wanafunzi hao 110 mjini Babati leo Jumatano Agosti 14, 2024 waliokwishawasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano kwa mchepuo wa Sayansi (PCM) na (PCB).
Amewaasa wasome kwa bidii na kutanguliza nidhamu kwa walimu ili waweze kutimiza ndoto zao na malengo yao ya baadaye.
Amewashukuru na kuwapongeza wazazi walioleta watoto wao katika shule hiyo mpya na kuwahakikishia kuwa watapata elimu na huduma bora, ulinzi na usalama wakati wote watakapokuwepo shuleni hapo.