RC Senyamule: Kinachoninyima usingizi ni uchumi wa Wananchi wa Dodoma

RC Senyamule: Kinachoninyima usingizi ni uchumi wa Wananchi wa Dodoma

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka Wataalam wanaoshughulika na usimamizi wa miradi ya maendeleo hususan miundombinu ya barabara, kuhakikisha inakidhi vipaumbele vya Mkoa wa Dodoma hasa katika kuinua uchumi wa wananchi wa Mkoa huu.

Snapinst.app_483281057_18043211954372730_1050373480794517546_n_1080.jpg
Hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha pili cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma 2024/2025, kilichofanyika Machi 06, 2025 katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Jengo la Mkapa Jijini humu ambacho kimelenga zaidi kujadili mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka mpya wa fedha 2025/2026.

Soma: Mkuu wa Mkoa wa Dodoma: Maadhimisho ya Kuzaliwa Kwa CCM 05 Februari, 2025 kutakuwa na uji bure kwa wananchi

"Sisi kama Mkoa, tunavyo vipaumbele ambavyo tunatamani miradi hii ivipe uzito stahiki, Wataalam tunaendelea na mchakato wa bajeti kwa sasa.Tunategemea kuona mabadiliko ya miundombinu hii
kuimarika kwenye Mkoa wetu lakini mwisho wa siku miundombinu ni uchumi, huduma za wananchi zitaimarika, na baadae uchumi wa wananchi utaimarika pia".


Snapinst.app_483012359_18043211972372730_7005094449618603510_n_1080.jpg
 
Dodoma imebarikiwa kuwa na zao la zabibu ambalo katika Afrika ni kwa Mandela tu inayo ikaribia

Chakushangaza maeneo yaliyopimwa na kutengewa kuzalisha Zabibu wamekuja wajanjawajinga kuyabadili matumizi kwakuweka makazi

Sasa hao ulio wawekea Makazi Wana Shughuli Gani kubwa ya kuongoza kipato

Je hayo mashamba yangewanufaisha watu wengi kwa muda mrefu

Kilichofanyika ni sawa na mgodi wa almasi wa Mwadui Shinyaga kubadili uwe Makazi

Nashangazwa na Nkuhungu broad acre kubadilishwa kuwa makazi wakati wakazi wenyewe hawatakuwa na Shughuli rasmi ya kuongoza kipato!!

Huo uwanja wa ndege Msalato ungebeba Zabibu kama Maua yanavyo bebwa Arusha!!

Tutafakari maamuzi ya haraka haraka mbona Nairobi kuna mbuga ya wanyama

Inashindikana nini mashamba ya Zabibu kuwa mjini?
 
Back
Top Bottom