RC Shinyanga apiga marufuku Watoto kutumikishwa mashambani, ataka wapelekwe Shuleni

RC Shinyanga apiga marufuku Watoto kutumikishwa mashambani, ataka wapelekwe Shuleni

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amepiga marufuku wazazi na walezi kuwatumikisha watoto mashambani na kuchunga mifugo badala ya kuwapeleka shule.

Msingi wa kauli ya Macha ni kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kusoma wanaandikishwa na wanahudhuria shuleni, akidokeza kuwa watakaokiuka watachukuliwa hatua.

Soma, Pia: Simiyu: Mwanafunzi adaiwa kufariki kwa kuchapwa viboko na kukanyagwa kichwani na mwalimu shuleni

Macha ameyasema hayo leo Jumanne Machi 4, 2025 katika hafla ya uzinduzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Bumva iliyopo Kijiji cha Bumva, Kata ya Segese, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala iliyojengwa kwa Sh603.9 milioni.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri hiyo, Rose Manumba amesema shule hiyo itawapunguzia umbali wanafunzi wa vijiji vya Bumva, Busongo C na Wisolele waliokuwa wanatembea zaidi ya Kilomita tano kuifuata Shule ya Sekondari Nyerere, hali iliyochangia kukithiri kwa utoro.

Shule hiyo mpya ina jengo la utawala, vyumba vinane vya madarasa, ofisi ya walimu, jengo la Tehama, maktaba, maabara tatu, vyoo na kichomea taka.
 
Back
Top Bottom