RC Sirro amewaonya wenye nia yakutenda uhalifu mkoa wa Kigoma

RC Sirro amewaonya wenye nia yakutenda uhalifu mkoa wa Kigoma

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP(Mst.) Mhe. Balozi Simon Sirro ametoa onyo dhidi ya wenyenia ya kutenda uhalifu mkoani humo na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo imara na halitosita kuchukua hatua dhidi ya yeyote atakayebainika kushiriki vitendo hivyo.

Soma, pia: UTEUZI: Balozi Simon Sirro ateuliwa kuwa RC wa Kigoma, Kenan Kihongosi kuwa RC wa Arusha. TRC yapata Mkurugenzi Mpya

Amesema hatofumbia macho vitendo vyovyote vya kihalifu mkoani humo huku akitoa wito kwa wenyenia ya kufanya vitendo hivyo kumrejea Mwenyezi Mungu na kuwa watu wema ili kudumisha amani na kuruhusu wakazi kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.

Chanzo:HabariMpya​
 
Niliona nchi fulani hapa wanamuita Mzee Tony Blair kama mshauri wao ndio nikaanza kuelewa jinsi tuliyo na tatizo la wazee washauri huku kwetu.
Sasa mstaafu mkuu inaelekea naye kachukua upande tayari hivyo ni kama hatoshi kuwa mshauri wa taifa la watu +65 million bali kundi la wakereketwa wasiozidi million 1.
Na hawa wengine ambao wangeshika nafasi za wazee washauri wa nafasi za kati na chini nao wanachukua upande.
Huwezi jua ni nani wa kuaminika tena au ndio tuendelee kuwategemea washauri wa kigeni!
 
Siro huyu ambae alishindwa kuwadhibiti panya road hapa Dar akiwa IGP wa polisi Tanzania nzima, ataweza kweli kuyadhibiti majambazi ya kihutu yaliojificha Kigoma kutokea Burundi?
 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP(Mst.) Mhe. Balozi Simon Sirro ametoa onyo dhidi ya wenyenia ya kutenda uhalifu mkoani humo na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo imara na halitosita kuchukua hatua dhidi ya yeyote atakayebainika kushiriki vitendo hivyo.

Soma, pia: UTEUZI: Balozi Simon Sirro ateuliwa kuwa RC wa Kigoma, Kenan Kihongosi kuwa RC wa Arusha. TRC yapata Mkurugenzi Mpya

Amesema hatofumbia macho vitendo vyovyote vya kihalifu mkoani humo huku akitoa wito kwa wenyenia ya kufanya vitendo hivyo kumrejea Mwenyezi Mungu na kuwa watu wema ili kudumisha amani na kuruhusu wakazi kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.
View attachment 3401631
Chanzo:HabariMpya​
😂😂😂
 
Ujanja ni kukamata Kwa Vitendo
Hutangazi kimya kimya wanedakwa
Alafu akishawakamata ndio aje atangaze kwamba tumewakamata Majambazi

Hapo maadui wanapata nafasi ya kujipanga
 
Back
Top Bottom