mdudu
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 7,013
- 10,000
Kufuatia kuuwawa kikatili kwa asikari wa JWTZ akiwa anatoka dolia ,kumeleta sintofahamu kwa wakazi wa mjini Tabora,
Mimi nikiwa raia mwema,nimesikitishwa na vitendo vya asikari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania kuwatembezea kipigo raia bila huruma kila wanaekutana nae tena bila kumpa hata nafasi ya kumhoji na kujitetea.mfano mimi nimetoka kijijini kwenye msiba wa mtoto wa kaka yangu aliyefariki siku sita zilizopita kwa kuumwa na nyoka.lakini hapo Jana nimefikia nyumba mojawapo ya kulala wageni ili asubui niendelee na safari kuelekea mikoa ya pwani ninapoishi baada ya kumaliza msiba,walifika asikari jeshi pamoja na polisi saa tano usiku,wakatutoa ndani ya vyumba watu 5 tuliokuwa tumelala hapo,
Bila hata kutuhoji,walianza kutupiga na kisha tukapelekwa kituo kikuu cha polisi Tabora tukiwa tumepigwa vibaya sana ,pamoja na mlinzi na wahudumu 4, tukiwa hapo kituoni alitufata mmiliki wa nyumba hiyo ya kulala wageni ,aliwasiliana na viongozi wa Polisi ndipo tukafanikiwa kutolewa lokap ,ilikuwa saa nane usiku,mmiliki wa nyumba yawageni akatueleza kuwa amewapa polisi shilingi laki moja ndiyo wametuachia,lakini tulikuta watu wengi sana wakiwa wamepigwa vibaya sana,
Kwanza sipingani au sifurahii juu ya unyama waliomfanyia asikari wa JWTZ hadi kumuua ,ni kitendo cha kinyama na cha kikatili walicho mfanyia asikari wetu akiwa anatoka kutimiza majukumu yake.Bali ni utalatibu mbaya unaotumika kuwabaini wahalifu,naamini Jeshi la polisi kwa kushilikiana na wananchi walio wema,wanaweza kabisa kuwabaini wahalifu wote,na siamini kama RC Tabora amewatuma wale asikari kuwapiga na kuwatesa kila raia wanaokutana nae.
RC ukiwa ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Tabora nenda kesho Lokap kituo kikuu cha polisi ukajionee mwenyewe raia walivyopigwa.
Nawasilisha