RC Tabora, ingilia kati kwa askari wa JWTZ kupiga raia ovyo

Hawa dawa yao ni kuwabeba kila mara kuwapeleza zile nchi zenye vita wakitoka uko wengine vilema na wengine wanarud kwenye masanduku akili ndo zitakaaa vizuri,,,sio kukaaa umu Tz kuzunguka zunguka ohooo mm mjeda sh@nZ kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana...njia wanayotumia siyo nzuri..hata kidogo..
 
Unadhani jeshi la uingereza au ufaransa wangefanya hivyo?
Jiulize tu jibu lako weka kichwani
 
Majeshi kuyachanganya na raia sio vizuri lazima migogoro itokee, ila kama wanakuwa kwenye makambi yao ambayo yako kwenye maeneo ya misitu inakukua sawa

Ila kutokana na nchi zetu za kiafrika unakuta bajeti yao haitoshi au fedha zao zinaelekezwa kwenye shughuli za wanasiasa ili kujitafutia kura basi migogoro ya Wanajeshi na raia haitakwisha
 
Majeshi yote polisi na JWTZ hawawezi kuwajibishwa wafanyalo ujinga endapo aliyefanyiwa ujinga ni mwananchi wa kawaida; Take it from me.
 
Natamani sana Sheria ya Nchi yetu kwa upande wa WAKUDA ingebadilishwa, au kuangaliwa upya.

Tatizo linalokuja ni kwamba, haitowezekana hata kidogo.

Ujue haya mambo ya kuisadia Polisi, au kosa afanye mwingine kisha mnakuja kujumuishwa aliyekuwemo na asiyekuwemo.

Kwa kweli ni kinyume na Haki za Binaadam
 
Kufuatia kuuwawa kikatili kwa asikari wa JWTZ akiwa anatoka dolia ,kumeleta sintofahamu kwa wakazi wa mjini Tabora,

Mimi nikiwa raia mwema,nimesikitishwa na vitendo vya asikari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania kuwatembezea kipigo raia bila huruma kila wanaekutana nae tena bila kumpa hata nafasi ya kumhoji na kujitetea.mfano mimi nimetoka kijijini kwenye msiba wa mtoto wa kaka yangu aliyefariki siku sita zilizopita kwa kuumwa na nyoka.lakini hapo Jana nimefikia nyumba mojawapo ya kulala wageni ili asubui niendelee na safari kuelekea mikoa ya pwani ninapoishi baada ya kumaliza msiba,walifika asikari jeshi pamoja na polisi saa tano usiku,wakatutoa ndani ya vyumba watu 5 tuliokuwa tumelala hapo,

Bila hata kutuhoji,walianza kutupiga na kisha tukapelekwa kituo kikuu cha polisi Tabora tukiwa tumepigwa vibaya sana ,pamoja na mlinzi na wahudumu 4, tukiwa hapo kituoni alitufata mmiliki wa nyumba hiyo ya kulala wageni ,aliwasiliana na viongozi wa Polisi ndipo tukafanikiwa kutolewa lokap ,ilikuwa saa nane usiku,mmiliki wa nyumba yawageni akatueleza kuwa amewapa polisi shilingi laki moja ndiyo wametuachia,lakini tulikuta watu wengi sana wakiwa wamepigwa vibaya sana,

Kwanza sipingani au sifurahii juu ya unyama waliomfanyia asikari wa JWTZ hadi kumuua ,ni kitendo cha kinyama na cha kikatili walicho mfanyia asikari wetu akiwa anatoka kutimiza majukumu yake.Bali ni utalatibu mbaya unaotumika kuwabaini wahalifu,naamini Jeshi la polisi kwa kushilikiana na wananchi walio wema,wanaweza kabisa kuwabaini wahalifu wote,na siamini kama RC Tabora amewatuma wale asikari kuwapiga na kuwatesa kila raia wanaokutana nae.

RC ukiwa ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Tabora nenda kesho Lokap kituo kikuu cha polisi ukajionee mwenyewe raia walivyopigwa.

Nawasilisha
Ukigusa tu vyombo vya Ulinzi na Usalama hapo hata uwe na haki utaikosa,usitarajie lolote hapo wewe uguza majeraha nenda nyumbani katulie!!!!
 
Jeshi letu limejaa vijana vilaza,wale rejects wa sekondali,ndio wamejaa jeshini,
Kuanzia viongozi wao,hawana akili,sasa ukipiga raia ndio utawajua wauaji!?badala ya kutumia njia za kisayansi,ufsnyike upelelezi,wao wanaenda manualy,kama vile muuaji ameandikwa usoni,tena unaweza kukuta muuaji yupo umo vikosini mwao,na ilikuwa kisa cha wivu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom