RC Tabora, ingilia kati kwa askari wa JWTZ kupiga raia ovyo

Mlipigwa na polisi? Au polisi pamoja na Jwtz? Polisi kukagua kwenye gesti na ili kujua kama kuna raia wema wageni wamefikia hapo ni jambo la kawaida. Sasa kama mlikuwa mmeandikiswa kwenye kitabu na vitambulisho mnavyo kwa nini wawakamate na kuwapiga?
 
Katika mikoa inayo ongoza kwa matukio ya ujambazi ni huo..maduka yote makubwa saa 12 jioni yamesha fungwa na kuna siku ilinisikitisha majambazi yalivamia kiduka cha mpesa saa 11 jioni yakampiga dada wa mpesa risasi akafa eti yakachukua laki 7.sa kweli laki 7 utoe uhai wa mtu.

Na mimi nasema wapigwe tu na usikute hiyo operation mkuu wa mkoa ana ijua maana ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa labda ukalalamike kwa jiwe.
 
Binadamu kwa asili aliumbiwa watu wawili, adui na rafiki, anaweza kuwa ni adui au rafiki anayeonekana au asiyeonekana kulingana na asili ya kuumbwa kwetu.

Kama nje ya ukoo au wanandugu hakuna adui basi basi miongoni mwao wenyewe hujikuta wanajenga uadui.

Taifa lisilo na amani kama Israel, jeshi lake humtafuta adui nje ya mipaka na raia wake huwa sehemu ya jeshi maana husaidiana na jeshi kumuwinda adui na hivyo mipaka ya jeshi ni ile iliyo mipaka nchi yao. Nchi yoyote yenye amani hukosa adui nje ya mipaka ya nchi yao.
 
na utakuta hao wauaji hakuna hata mmoja aliekamatwa, wameshahamia mkoa mwingine wanaendelea na maisha yao, wanaopata shida ni wengine wasio na hatia, wangefanya upelelezi kwa weledi
Hao raia walioua ni ndugu zao, wanaishi kwenye majumba yao, kwenye mitaa yao kichapo kitembee mpaka wataje Vibaka wote, Mwanajeshi hawezi kuuliwa kizembe kizembe halafu wenzake wakae kimia ebboooo.

Waweza kuta ni Vijana wenzake wa Tarime wameamua kulianzisha tu hata siyo kikosi kizima maaaana Mkurya kwa Kulipa kisasi cha Mauaji ni sawa na Sawa na Mmasai na Kirungu.

RIP Soldier Vijana wenzako wamekutendea haki kwa kufikisha Uchungu na Ujumbe kwamba Dawa ya Moto ni Moto.
 
Jamii ngumbaru hiyo mleta uzi usitegemee la maana hapo.
 
Màoni kama haya hutolewa na watu wakatili tu, ambao hata utu hawana. Siju katika maisha yako kama umewahi pigwa.

Hivi wewe unajikuta watu wanakupiga, hujawahi Fanya uhalifu katika maisha yako yote na wewe ni tegemeo la familia, pengine unapewa kilema cha maisha utajisikiaje?

Kumbuka hawa wanaokupiga bila sababu ni vijana wetu, wemepelekwa mafunzo kwa ajili ya amani yako, wamelipwa pesa yako kwa ajili ya amani yako, wamekabidhiwa bunduki yako kwa ajili ya amani yako.

Kwa sababu tu ya vibaka wachache ambao polisi wana uwezo wa kuwatafuta, usalama wa taifa wana uwezo wa kuwatafuta, wewe unapewa kilema hiyo ni haki kweli? Nani sasa atakuwa mlinzi wa amani yako?
 
Nguvu za kupigwa na raia Hadi kufa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kkwani wameshindwa kufanya investigation ya kitaaluma kupata wahusika kama wanavyo fanya kwenye matukio mengine?

Sasa unapo piga kila raia unaye muona ndio umetatua tatizo na kumpata muhusika?

Kwani askari wanaua raia mara ngapi ? Tena bila hata hatia? Je na wao wawe wanavamiwa na kupigwa hovyo hovyo?

Ifike mahali waanajeshi wa tanzania na vyombo vyote vya ulizi viache kuamin kwamba viko juu ya sheria na na vina uhuru wa kufanya vyovyote watakavyo bila kuchukua hatua na hivyo ndivyo wanavyo pandikiza chuki zaid

Kama na wewe ni askari na una mawazo kama hayo basi ni hakika tuna jeshi lisilo tumia akili

Jifunzeni kwa wenzenu wanafanyaje kazi na hasa inapo tokea tukio kama hilo sio kutumia nguvu kwa kupiga kila raia naye onekana hiyo inasaidia nini? Zaid ya unyanyasaji na kuzidisha chuki zaid?

Askari wengine eti kwa vile mdemu anaye mtaka yeye kuna raia ana mahusiano naye basi hakawii kumtengenezea kesi yaani ujinga ujinga ujinga
 
Askari wa bongo ni mlenda tu unapigwaje na raia hadi kufa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…