RC Tanga: TRA acheni kujenga Mazingira ya chuki kwenye ukusanyaji wa kodi

RC Tanga: TRA acheni kujenga Mazingira ya chuki kwenye ukusanyaji wa kodi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amewataka watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wafanyabiashara mkoani humo, kutojenga mazingira ya chuki wakati wa ukusanyaji kodi.

Alitoa jana rai hiyo wakati wa kikao cha wadau wa kodi, ambao alisema kuwa iwapo pande zote mbili zitafanya kazi kwa uwazi bila ya kificho, hakuna umuhimu wa uwepo wa uhasama wala chuki baina yao.

Alisema kuwa kodi ndio uti wa mgongo wa taifa lolote, kwa hiyo ni lazima kujipanga vizuri kuhakikisha kwamba watumishi TRA na wafanyabiashara hawajengeani mazingira ya chuki, kwa kudhani kwamba wafanyabiashara ndio wanakwepa kodi au watu wa TRA wanakuja na makadirio yasiyokuwa na utaratibu.

Alitaka watumishi kufanya kazi kwa kufuata kanuni za utumishi wa umma zinavyoelekeza na wafanyabiashara wafanye shughuli zao kwa utaratibu mzuri.

“Hakuna sababu ya kuibiana wakati mifumo ya ukusanyaji imetengenezwa na inafanya kazi kwa utaratibu, hivyo tunaweza kukusanya kodi kwa ufanisi na kufikia malengo tuliyojiwekea,” alisema Mkuu wa Mkoa.

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Specioza Owure alisema bado wanaendelea kutoa elimu ya kodi na umuhimu wa wafanyabiashara kutoa risiti wakati wa kuuza bidhaa kwa mteja.

Alitaja changamoto kubwa ilipo ni bado wananchi wengi hawana utaratibu wa kudai risiti wanapofanya manunuzi. Alisema kudai risiti ni haki yao.

“Wananchi wajenge tabia ya kudai risiti kwani hiyo inaonyesha uzalendo kwa nchi yao. Unapodai risti nawe unakuwa sehemu ya walipa kodi, naomba wafanyabiashara kujenga tabia ya kulipa kodi kwa hiyari,” alisema.
 
Kuna afisa TRA Morogoro ana uwalaza mtu mzima lakini blazamen balaaaa, laiti wote wangekuwa kama yule tra ingekuwa sehemu salama Sana ya kufika kwanza anakufanya ujisikie una haki ya kulipa Kodi kwa lugha ya staha kwa alivyo alipaswa aringe kweli lakini he is so amazing kwakweli sijui bado yupogi pale.
 
kuna afisa tra morogoro ana uwalaza mtu mzima lakini blazamen balaaaa,laiti wote wangekuwa Kama yule tra ingekuwa sehemu salama Sana ya kufika kwanza anakufanya ujisikie una haki ya kulipa Kodi kwa lugha ya staha kwa alivyo alipaswa aringe kweli lakini he is so amazing kwakweli sijui bado yupogi pale
Vitu vzr havidumu aisee, usishangae ameshapigwa majungu na kutemeshwa mzigo tayari.
 
Kazi ya TRA ni kukusanya kodi na kumjenga mlipa kodi aweze kukua kwa mapato zaidi.
 
kuna afisa tra morogoro ana uwalaza mtu mzima lakini blazamen balaaaa,laiti wote wangekuwa Kama yule tra ingekuwa sehemu salama Sana ya kufika kwanza anakufanya ujisikie una haki ya kulipa Kodi kwa lugha ya staha kwa alivyo alipaswa aringe kweli lakini he is so amazing kwakweli sijui bado yupogi pale
Sasa character za watu wa aina hiyo ni chache sana. Wengi ni wazee wa force.. hila hila tu
 
TRA moshi wamevamia club maarufu ijulikanayo kama Rau pub usiku na kuifunga wakidai club hiyo inadaiwa hivyo wanatakiwa kufunga na kulipa kwanza, hali iliyopelekea tafrani ,maana wateja bado walikuwa wamejaa sana!

Umetokea mvutano mkubwa kati ya meneja wa pub hiyo na TRA akidai inakuwaje waje usiku? Wakamjibu wameagizwa na boss Mkoa
Means walikuwa targeted.

Wanataengeneza mazingira ya rushwa na kubambikia kesi.

Sio professional conduct.

Kama bar/pub ni jengo means lipi hapo na wanafanya kazi asubuhi to usiku. Kitendo cha kuvamia usiku ni dalili tosha kuna kitu zaidi jikoni i.e. TRA na Polisi.

Hizi mamlaka zinatumika vibaya sana.
 
Sasa character za watu wa aina hiyo ni chache sana. Wengi ni wazee wa force.. hila hila tu
kabisa aiseeeeeeeeee kama Kuna limama lina matege hv Lina roho mbaya Kama sura yake ilivyo aiseeee,customer care ilipaswa ianzie kwa Hawa watu aiseeee
 
Vijana wengi TRA ndiyo wenye matatizo sababu ya tamaa ya utajiri wa haraka so frustrating kwa wafanya biashara. Wapewe elimu ya maadili ya utumishi wa umma
 
Back
Top Bottom