Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,513
Kanuni kuu ya kimaadili kwamba, malengo mazuri hayapaswi kuhalalisha mbinu haramu, ni kanuni ya kweli siku zote, sehemu zote na kwa watendaji wote.
Ni kwa sababu hii tunasema kwamba, vyombo vya dola havina mamlaka ya kuzuia uhalifu kwa kufanya uhalifu.
Lakini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, na washauri wake, wanayo mawazo tofauti na haya.
Juzi Chalamila aliahidi kuvunja haki za raia na ametekeleza azima yake kupitia jeshi la polisi.
Alitamka kwamba wanaotaka kukinukisha atahakikisha wananuka wao. Kumbe alimaanisha kuteka, kutesa, kuvunja mikono, kuvunja miguu na kumwaga damu.
Viongozi wa Chadema wamewekwa kizuizini makao makuu ya Chama MIkocheni, vijana wametekwa, kupigwa na kutupwa misitu ya Bagamoyo na Mabwepande, kuna waliovunjwa miguu na mikono, wengine wamepasuliwa mafuvu kwa virungu.
Utetezi wa RC Chalamila ni kwamba vyombo vya dola vilikuwa vinatekeleza jukumu lake halali la kuzuia uhalifu.
Lakini jeshi hilo limejaribu kuzuia kinachoitwa uhalifu kwa kufanya uhalifu.
Haki za kikatiba zilizovunjwa na jeshi la polisi katika operesheni ya kuzuia wfuasi wa Tundu Lissu wasifike mahakamani ni pamoja na:
- Haki ya kwenda popote nchini, ikiwa ni pamoja na mahakamani;
- Haki ya kila mtu kuhesabiwa mtakatifu mpaka hapo tuhuma dhidi yake zinapothibitishwa na chombo huru;
- Haki ya utu wa kila mtu huheshimiwa kabla, wakati na baada ya mchakato wa haki jinai.
Hizi ni haki tulizopewa na Mungu.
Haki hizi hazikutokana na hisani ya serikali.
Haki hizi hazikutokana na hisani ya chama tawala cha CCM.
Tume ya Haki za BInadamu Mnasemaje?
Rais Samia aliyeapa kuhifadhi katiba ya nchi anasemaje?
Waziri wa utawala bora yuko wapi?
Bado RC Chalamila yupo ofisini?
Bado Waziri wa mambo ya ndani yuko ofisini?
Bado Tanzania ni Jamhuri au sasa rasmi imegeuzwa dola ya kisultani chini ya Rais Mwarabu?
Bado kuna shaka tena kuhusu dhana kwamba ile nakishi ya kidemokrasia (democracy deficit) iliyoko kwenye mataifa yote ya kisultani huko Uarabuni sasa imehamia nchini Tanzania kwa sababu tu tunaye Rais Mwarabu?
Bado kuna Mtanzania anayekataa rai kwamba hakuna Mwarabu anayeweza kuwa Rais bora katika dola ambayo inaongozwa kwa kufuata kanuni za Jamhuri?
Mwenye macho haambiwi tazama simba anakuja!
Sasa serikali inatumia kisingizio cha "preventive justice" kubadilisha Katiba kwa kufuta vifungu vya kikatiba vinavyoongelea "presumption of innocence"
Hapana.
Serikali haina mamlaka hayo.