RC wa Morogoro Adam Malima achimba mkwara mzito kuwafuta kazi watendaji wa MORUWASA baada ya malalamiko kuwa mengi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mbona vitisho vimekuwa vingi sana kipindi hiko cha karibuni? Yaani kila mtu anamtisha mnyonge wake.

Kuna nini?

========================================================

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima ametishia kuwahamisha baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (MORUWASA) baada ya kuzidi kwa malalamiko ya ukosefu wa huduma ya maji ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Malima amezungumza hayo katika kikao cha kamati ya Ushauri ya mkoa na kuongeza kuwa hafurahishwi na majibu ya watendaji hao juu ya suluhu ya adha ya uhaba wa maji kwa wananchi mkoani humo.

Source: Manara TV
 
Kila mtu na mnyonge wake!
Uongozi wa kufokafoka, kukaripia na kupigana biti
 
Wakuu,

Mbona vitisho vimekuwa vingi sana kipindi hiko cha karibuni? Yaani kila mtu anamtisha mnyonge wake.

Kuna nini?

========================================================

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima ametishia kuwahamisha baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (MORUWASA) baada ya kuzidi kwa malalamiko ya ukosefu wa huduma ya maji ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Malima amezungumza hayo katika kikao cha kamati ya Ushauri ya mkoa na kuongeza kuwa hafurahishwi na majibu ya watendaji hao juu ya suluhu ya adha ya uhaba wa maji kwa wananchi mkoani humo.

Source: Manara TV
Bangi zake tu huyo hana uwezo huo
 
Baada ya miaka 60 ya uhuru bado kuna shida ya maji 🥱🥱
Leo nimepiga namba ya MORUWASA Huduma kwa wateja (0800751011) Nashangaa naambiwa "NAMBA ULIYOPIGA SIYO SAHIHI TAFADHALI HAKIKI KABLA YA KUPIGA TENA"
Nikadhani shida ni Mtandao! nimejaribu siku nzima majibu ni yaleyale. Ngachokaa!
 
Back
Top Bottom