Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Kwanza sikiliza hii
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongela, ni moja wa Ma RC very bold katika kuusema ukweli bayana!, leo amevunja mwiko wa ukimya kwa viongozi wa serikali kutompigia kampeni zozote za kisiasa kwa mgombea yoyote, kwasababu hawa ni viongozi wa kiutendaji, lakini RC John Mongela, amevunja ukimya wa kumhusu JPM, kwa kuusema ukweli wa moyo wake kuwa bila Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Tanzania, tusingefika hapa tulipo!, huo ndio ukweli wa mambo.
Mongela amesisitiza na hapa nina mnukuu, "Sisi ni Watanzania, lazima tuwe wazalendo, kwenye mambo ya msingi, hatuwezi kuwa na aibu kusema, tunasemea nchi yetu, tunasemea mustakabali wa kizazi chetu na vizazi vingine vijavyo, wazee waliotangulia walitimiza wajibu wao, na sasa tumepata kiongozi mzalendo mahiri, ambaye amejitoa sadaka kwa ajili ya nchi yetu, tuendelee kumuombea, lakini tarehe 28 October, mimi nikiwa kama kiongozi, niwaombeni tutoke, tukapige kura, ili Mhe Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kama miaka mitano ilikuwa hivi, tukimpa tena miaka mitano mingine, itakuwaje?, na walioona kitabu cha ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, na mimi kwa nafasi yangu ndio mratibu na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa ilani kwenye mikoa, tunakokwenda ni nchi ya maziwa na asali, tumuombee rais wetu, tumuunge mkono, tukapige kura, ili twende kwenye mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii!.
Akiunga mkono hoja, mwandishi wa makala hii, alisisitiza, umuhimu wa waandishi wa habari na vyombo vya habari, kutoshabikia vyama wala wagombea, ila amesisitiza, kama tunataka maendeleo ya kweli, then, tunajua ni chama gani kinaweza kutuletea maendeleo ya kweli na sio ahadi, na ni mgombea gani anaweza kutuletea maendeleo ya kweli, hivyo tarehe 28, Watanzania, Tusifanye Makosa!.
Paskali