impongo
JF-Expert Member
- Feb 18, 2015
- 8,764
- 7,758
Sasa hivi nimekupuuza [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongela, amevunja mwiko wa ukimya kwa viongozi wa serikali kutompigia kampeni zozote za kisiasa kwa mgombea yoyote, kwa kuvunja ukimya, kumhusu JPM, asema bila Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Tanzania, Tusingefika hapa tulipo!, huo ndio ukweli wa mambo. "Sisi ni Watanzania, lazima tuwe wazalendo, kwenye mambo ya msingi, hatuwezi kuwa na aibu kusema, tunasemea nchi yetu, tunasemea mustakabali wa kizazi chetu na vizazi vingine vijavyo, wazee waliotangulia walitimiza wajibu wao, na sasa tumepata kiongozi mzalendo mahiri, ambaye amejitoa sadaka kwa ajili ya nchi yetu, tuendelee kumuombea, lakini tarehe 28 October, mimi nikiwa kama kiongozi, niwaombeni tutoke, tukapige kura, ili Mhe Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kama miaka mitano ilikuwa hivi, tukimpa tena miaka mitano mingine, itakuwaje?, na walioona kitabu cha ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, na mimi kwa nafasi yangu ndio mratibu na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa ilani kwenye mikoa, tunakokwenda ni nchi ya maziwa na asali, tumuombee rais wetu, tumuunge mkono, tukapige kura, ili twende kwenye mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii!.
Akiunga mkono hoja, mwandishi wa makala hii, alisisitiza, umuhimu wa waandishi wa habari na vyombo vya habari, kutoshabikia vyama wala wagombea, ila amesisitiza, kama tunataka maendeleo ya kweli, then, tunajua ni chama gani kinaweza kutuletea maendeleo, na ni mgombea gani anaweza kutuletea maendeleo ya kweli, hivyo tarehe 28, Watanzania, Tusifanye Makosa!.
Paskali
Aisee siasa mbaya sana nawewe tumekupoteza kwa heri