Baada ya kufanikiwa kusalia kwenye NBC Premier League, hatimaye Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amewakabidhi wachezaji wa Tabora United, kitita cha Shilingi milioni 50 aliyowaahidi endapo wangefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu Bara.
Tabora United imesalia NBC Premier League baada ya kuifunga Biashara United ya Mara, kwa jumla ya magoli 2-1 kwenye michezo yote miwili ya mtoano (play offs).
Msimamizi wa timu hiyo ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richald Abwao amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Tabora na mashabiki wao kuwa msimu ujao wanakwenda kufanya makubwa zaidi kulingana na changamoto walizopitia sasa wanakwenda kufanyia masahihisho na kuja kivingine nyuki wa Tabora.
Aidha, Abwao ameeleza "Msimu ujao hawaendi kushiriki bali wanaenda kuonesha upinzani kwa kila timu itakayo kuja mbele yao jukumu ni moja kushinda ndilo jukumu lililo mbele yetu."