Re: Jaman huu utaratibu wa English Medium Schools na Waalim wao Vipi?

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
10,568
Reaction score
9,710
Ningependa kupata ushauri kwa wenye watoto kwenye shule hizi.Kiafya,kisaikolojia na kiakili

Nitaongelea kuhusu
a)Muda wa shule (b)Muda wa kupumzika(c)Home works (d)Weekend works(Holiday Packages)
e)Ada kubwa waalim wavivu

Mtoto inabidi amke saa kumi na moja na nusu kwa baadhi ya maeneo.Na anatoka shule saa tisa na kufika nyumbani saa kumi na mbili jioni.

Hapo unakuta mtoto kutwa nzima hajalala,na nielewavyo mie kipindi cha ukuwaji wa mtoto ulalaji hasa wa mchana ni bora sana kwa afya yake na Afya ya akili kwa ujumla.Na ukizingatia kaamka alfajiri.

Hapo napima kuhusu uelewa wa mtoto kwa masomo ya mchana kama anakamata kitu.

Na wakati huo anafika nyumbani saa kumi na mbili ana home works telee,karibu karatasi tatu in full kila siku.

Sasa hapa ndio najiuliza,muda aliomka na muda wa kurudi na muda wa kufanya home works nyingi namna hiyo tena on daily basis.Kweli hapo kichwa kinakuwa sawa?na je muda gani atapata wa kurejea masomo ya nyuma,yaani hata kama umempangia Time Table ya kujisomea Nyumbani haiwezekani kabisa.Akimaliza Home works ni kula kisha ni kulala tu kwa mchoko.

Maana kila akirudi ana home works kibao,na ikifika mtihani inabidi sasa ndio arejee masomo ya nyuma kwa kukariri,maana alikuwa hanamuda wa kufanya rejea.

Huu wingi wa Home works nahisi kama ni uvivu wa waalim kufundisha,wanakula pesa ndefu lakini hapa naona kama ni kutegea,wanajua mzazi upo nyumbani utamsaidia majukum,hili sio tatizo ila sio kwa kiwango hiki kwa kila siku.

Na ikifkia weekend basi ni booklet nzima ndio home work.

Mwisho wa siku inakuwa ni kumuwekea mazingira ya mtoto kukariri tu kwa ajili ya mtihani na sio kuelewa.

Maana hana muda wa kufanya rejea ya msomo ya nyuma.Angalau Home works zingekua zinatolewa weekends tu ili katikati ya wiki mzazi apate muda wa kumwekea mwane ratiba ya kusoma na kumsimamia, hata kama anatoka mida hiyo angalau kwa lisaa limoja apate kufanya rejea,lakini kilasiku home works karatasi tatu,

Hembu naoma tushauriane hili hasa kwa upande wa Afya ya mtoto na akili under 10yrs.
 
kweli kabisa, watoto wadogo hawahitaji home work ili kukua , wanahitaji kucheza zaidi ili kuweza kujitambua na kukuza ubongo wao. wanatafuna pesa tuu za bure
 
Mtoto mpeleke english medium iliyo karibu tatizo unampeleka shule karibu km 15 na zaidi.lazima gari ipite mapema na achelewe kurudi.akienda shule ipo karibu gari haiwezi kumpitia asubuhi sana na hawezi kuchelewa kurudi na atapata muda wa kutosha kufanya home work pomoja na kucheza na mambo mengine.wazazi ndo wanachosha watoto kwa kuwapeleka shule za mbali
 
Duuh. wewe umetoa mpya kabisa. Kwamba walimu ni wavivu kwa kutoa home works kwa watoto? Ukimaanisha kuwa waalimu ambao hawatoi home works kwa watoto ndo wachapa kazi?
 
Hizi Shule ni pasua kichwa kabisa na nadhani ni Msiba na Janga jingine kwenye mfumo wa Elimu yetu hapa Tanzania. Kwanza masomo wanayofundishwa utakuta hayaendani na level yao ya kidarasa na kiakili,imagine Mtoto wa STD five ameshasoma na kumaliza ile Topic ya Reproduction ya form three sasa sijui hapa kuna faida gani?. Pili hizi shule kwa outings za kwenda sijui Beach na Mbugani ndio zinaongoza. Tatu watoto kupewa H/W zilizo juu ya uwezo wao,utakuta Mtoto amepewa H/W ya masomo 3 na zote hazipungui uchache wa maswali 20 kwa kila somo na kilichoniacha hoi ni pale Mtoto alipopewa H/W ya swali moja then jibu la hilo swali alirudie kuliandika mara Mia Moja,sasa hapa ni kumfundisha Mtoto au kumkomoa?

Mimi nashauri Serikali iingilie kati kwa hili hasa kuhusu Mitaala wanayotumia hawa watu,kwanza utakuta Shule inafundisha Asilimia 95 kwa kutumia lugha ya Kiingereza na Kifaransa,wakati kwenye Mitihani ya Taifa i.e STD na Seven lugha inayotumika kwa Asilimia 95
 



mpeleke shule za kayumba awe anapumzika huko hakunaga ma hworks ni vishert kwa kwenda mbele kazi ni kumpa mfagio na dumu la maji

asikudanganye mtu nchi nyingi za kiafrika elimu yetu ni ya kukalili tu wewe huwezi kusoma masomo kumi na moja na ukaelewa yote


kama mtoto hafanyi home works kibongobongo hawezi toka kumbuka watoto hawana muda wa kujosomea kiumri na kiakiri kulingana na umri wao wa michezo

kama unabisha fanya haya

nenda shuleni kwao uwaambie walimu wasimpe mtoto homeworks then usimwambie kusoma uone :wanamichezo mia kwa siku hawa jamaa
 
kweli kabisa, watoto wadogo hawahitaji home work ili kukua , wanahitaji kucheza zaidi ili kuweza kujitambua na kukuza ubongo wao. wanatafuna pesa tuu za bure

we ni mwalimu? Umesoma malezi ya ukuaji na ufundishaji watoto kama hujui uliza usikirupuke kama mlugo be smart
 


et unakuta baba zima na madegre yake linaishi mbezi ya kimara mtoto anasoma upanga very silly
 
Duuh. wewe umetoa mpya kabisa. Kwamba walimu ni wavivu kwa kutoa home works kwa watoto? Ukimaanisha kuwa waalimu ambao hawatoi home works kwa watoto ndo wachapa kazi?



matatizo ya kuwapenda watoto kupitiliza haya hadi unamwonea huruma kusoma
 


mfumo wa elimu umekua mkuu wewe elimu ya uzazi ndio imekuchanganya mbona huulizi ma ict na mengine kibao.waachani watoto wasome
 
Mahitaji yote yanapatikana shule asubuhi wana soma mchana wanakula wakishakula wanalala karibia kila shule ina sehemu na magodoro ya kulalia wakishaamka wanacheza jioni wanarudi kwao.
 
kweli kabisa, watoto wadogo hawahitaji home work ili kukua , wanahitaji kucheza zaidi ili kuweza kujitambua na kukuza ubongo wao. wanatafuna pesa tuu za bure

Shule nyingi zina michezo ndugu mngejaribu kuspend walau siku moja kwenyeshule husika mkaona ratiba zao jamani.. kiufupi wanaratiba kushinda hizi za serikali kila siku wanatatiba ya michezo na kulala kabla hawajarudishwa majumbani.
 
Mi naomba kuuliza tu kwa wenye ufahamu, kwakuwa hili somo la kifaransa halipo kwenye mtihani wa Taifa mimi kama mzazi naweza kuuomba uongozi wa shule kwamba mtoto wangu asisome somo hilo?

maana nina uhakika na ushahidi hata waalimu wanaofundisha kifaransa hawaijui lugha hiyo zaidi ya ujanjaujanja tu na kama nitahitaji mtoto ajuwe kifaransa basi navijuwa vyuo special vinavyofundisha lugha tu. Hili swali langu msingi wake ni kumpunguzia mtoto rundo la masomo ambayo hayana maana yoyote na kumbebesha mzigo usio wa lazima.
 

Mitihani ya STD 7 ipo ya aina mbiki ndugu hata ya std 4 pia ipo ya kiingereza na kiswahili ila mtihani ni huohuo unakuwa lugha mbili ndo maana hata kitaifa matokeo yanajumuishwa shule zote private na govt na hata selection za form one wote wanachaguliwa za serikali za kata na zile kongwe sema tu privaye wengi wanawapeleka shule za private tena na si za serikali. Ingawa wapo watoto wengine waliosoma english medium primary lakini Olevel wanadoma shule za kata hawa ni wale ambao wazazi wao wameshindwa au kuanguka kiuchumi na kukosa uwezo wa kuwaendeleza shule za private.


Kuhusu mitaala ya kiingereza haijaanza leo kumbuka kunashule za serikali pia ambazo zipo katika mfumo wa english medium tangu enzi hizo mpaka sasa mf. Olympio, Diamond na Arusha school hizi ni Kayumba zinamilikiwa na serikali ila zinafundisha mfumo wa Kiingereza tangu zimeanzishwa.
 

unamaana asifundishwe yeye peke yake shule nzima yaani mwalimu akiingia darasani mwanao atolewe nje:
 
Watanzania tutaendelea kuwa nyuma kwa uvivu wa kufanya utafiti. Huwezi kutoa lawama kwa kuangalia tatizo la shule moja tu, umechunguza na shule zinginezo na kuona tatizo hilohilo?
Elimu kwa sasa imekuwa na pia ni ya ushindani, usitegemee eti kwa kuwa ww ulisoma riproduction form three basi na mwanao nae afanyiwe hivyo, huo ulikuwa ni uvivu na uhaba wa walimu wako wa primary... acha watoto wakuzwe katika misingi inayofaa, kama michezo na kulala ipo kwenye shule nyingi tu za aina hiyo.
Fanya utafiti mkuu acha kulalama bureeee
 

Nnavojua shule hizi ukiacha zile za international zina mtaala mmoja na wa serikali tofauti yake ni lugha ya kutekelezea.
 
mfumo wa elimu umekua mkuu wewe elimu ya uzazi ndio imekuchanganya mbona huulizi ma ict na mengine kibao.waachani watoto wasome

Acha ujinga wewe,Watoto kuwa overloaded na H/W na masomo kuliko saizi yao na kusoma hizo shule za English Medium ndio mfumo wa Elimu kukua?hizi zero zinazongezeka kila Mwaka kwa form 4 na watoto kwenda Form One pasipokujua kusoma wala kuandika ndio mfumo wa Elimu unakua?mbona hizo English Medium haziongozi au kufanya vizuri kwenye Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba zinazidiwa na Shule za St.Kayumba.
 
Nnavojua shule hizi ukiacha zile za international zina mtaala mmoja na wa serikali tofauti yake ni lugha ya kutekelezea.

Hiyo Mitaala ni formality tuu Mkuu,but ukifanya uchunguzi nini kinachofundishwa huko ndio utajua ninachoongea,kwanza Vitabu vile vya Ithibati na Mazoezi wanavyotumia ni tofauti kabisa na vile vya Serikali,wengi wanatumia Vitabu vya Mitaala ya India na Kenya,sasa hapa Mtoto huyo huyo aje kufanya Mtihani mmoja na watoto wa Shule za St. Kayumba,what did you expect?. Kwenye swala la lugha tuu kiukweli wapo vizuri,kama the Chair,the Table hapo watoto wa Kayumba watasubiri sana but kwenye General knowledge watasubiri sana dhidi ya Watoto wa Kayumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…