Read Between The Lines: Yanga SC Wanaitwa Kijanja Mezani na Azam FC

Read Between The Lines: Yanga SC Wanaitwa Kijanja Mezani na Azam FC

Azam wamalizane na dude walilolitengeneza wao wenyewe...
 
Rudia tena kuisoma hiyo taarifa Mkuu, hiyo imekaa kwa mtindo wa kama kumkomoa Dube alazimishwe kwenda asikopataka.

Hapo kwa timu hizo mbili chaguo lake ni Simba tu, kwa sababu Dube hawezi kuwa tayari kwenda kucheza vitani hata iweje.

Na kwa kuwa Yusuph Bakhressa ni mwanachama wa Simba, hiyo ofa anaitoa mwenyewe tu, ni kama Dube anaenda bure Simba.

Hata Yanga wakipeleka ofa, utasikia Simba wamepanda dau. Mwisho wa siku akacheze Simba na siyo Yanga walioanzisha hii 'sinema'.

Ila, yote kwa yote muda utasema kila kitu. Tujipe muda, ila kwa sasa picha ndiyo hiyo.

Ova
B… Na akili zako zote ila likija suala la Simba huwa unaziweka pembeni unakuwa shabiki kama Kisugu.

Wakati wa Feisal si alionekana ana haki kutaka kuvunja mkataba? Kwanini iwe tofauti Dube akitumia njia ileile?

Hiyo unayoita sinema waasisi ndio hao wanaohaha sasa hivi.
 
Wala sijasema kwa sababu ni shabiki wa Simba, na wala siwalaumu Yanga hata kidogo. Haya mambo ndiyo utamu wenyewe wa ushabiki wa soka.

Ujanja wa ndani na nje ya uwanja wa kugusana panapouma, ndiyo tofauti ya soka ba michezo mingine. Iwe kwenye usajili au kwenye mechi zenyewe.

Yanga waliwahiwa wakati ule, kisha nao wakaja kivingine kwa kisasi. Ndiyo soka b..., ndiyo maana makosa ya waamuzi hayaishi viwanjani. Ujanja kuwahi ndiyo soka.

Ova
 
Back
Top Bottom